Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Tanga umezindua rasmi Tanga ya kijani.

Akizungumza katika hafla hiyo mgeni rasmi mwenyekiti UVCCM Taifa Ndugu Kheri James amewaasa vijana kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.

Aidha, mwenyekiti huyo wa UVCCM Taifa kwa niaba ya Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi Tanzanian amempongeza Mh. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuaminiwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi zilizo kusini mwa Africa (SADC) hakika ameendelea kuiheshimisha nchi yetu.

Nae, Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Tanga Ndugu Omary Mwanga amewashukuru wote waliojitokeza kushiriki tukio hilo. Hakika jambo limeonekana.

Waziri Mohamed
Katibu Hamasa na Chipukizi
Mkoa wa Tanga
Share To:

msumbanews

Post A Comment: