Na Lucas Myovela_ARUSHA


Tume ya Nguvu za Atomic Tanzania ( TAEC ) imetoa elimu ya upimaji wa kiasi cha chembechembe za mionzi kilicho ingia mwilini ili kunusulu watanzania dhidi ya madhara ya mionzi yanayoweza  kusababisha majonjwa kama ya  kansa yanayo sababishwa na mionzi.


Peter Ngamilo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TAEC akiaongea na wananchi kwenye maonesho ya 26 nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Taso njiro jijini  Arusha akitoa elimu, alifafanua juu ya  kazi ya mtambo maalumu wa upimaji kiasi cha mionzi kilichoingia mwilini (Whole Body Counter)


Bw  Ngamilo ameleza kwamba mpaka sasa toka maabara mpya ya TAEC izunduliwe na Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania April 29 mwaka huu mtambo huo umeshaanza kufanya kazi na kuwa na matokeo chanya kwa wananchi.


"katika utumiaji mitambo hii kwenye upimaji wa chembe chembe za miomzi hazima madhara yeyote kwa binadamu hasa wale wanapimwa kiasi cha chembe chembe mwilini na sisi kama TAEC  gharama zetu ni nafuu sana katika upimaji ya mionzi mwilini." Alisema Ngamilo.


Watu wengi wanaofanya kazi katika viwanda,Secta ya Afya,Ujenzi, Tafiti pamoja na wachimbaji wa migodi hawa wote wapo hatalini kuingiliwa na mionzi mwilini endapo watafanya kazi zao katika mazingira yasiyo salama." Aliendelea kueleza Ngamilo


Mbali na utoaji wa huduma hii ya upimaji wa chembe chembe za mionzi mwilini tasisi hii ya TAEC inahusika na udhibiti matumizi salama ya mionzi hapa nchini,kuhamasisha na kuendeleza matumizi salama ya Taknolojia ya Nyuklia,kufanya tafiti na kutoa ushauri na taarifa mbalimbali juu ya Sayansi na Tknolojia ya Nyuklia,Pia uzalishaji wa mbegu za wanyama zilizo bora pamoja na Mimea.


Tasisi hii ya TAEC ilianzishwa kwa sheria ya Bunge namba 7 mwaka 2003, huku awali ilikuwa ikijulikana kama Tume ya Taifa ya Mionzi iliyo anzishwa kwa sheria ya Bunge namba 5 ya mwaka 1983,Lengo kuu likiwa ni kudhibiti matumizi salama ya mionzi ili kulinda umma.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: