Na Thabit Hamidu,Zanzibar.

Vijana nchini wametakiwa kutotumika vibaya na kujiingiza katika vitendo vya uvunjifu wa amani na badala yake kubadili mitazamo kwa kuzitumia fursa zilipo na kushiriki shughuli za kiuchumu ikiwemo Ujasiriamali.

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mheshimiwa Ayoub Mohammed Mahmoud ametowa wito huo wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa vijana kuhusu ubalishaji tabia na kuwaongezea uwezo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya PYDOZ yaliyofanyika katika ukumbi wa ABLA Beit el Ras Wilaya ya Magharibi A.

Amesema wakati umefika kwa vijana kujitambua na kubadili mawazo na mitazamo hasi kwa kuwa wabunifu na kuzitumia fursa zinazowazunguka kwa kujimarisha kiuchumi na kujijengea hatma ya maisha yao na kukuza maendeleo nchi.

"Uzoefu unaonesha katika nchi nyingi duniani chanzo kikubwa cha migogoro ni kutumika vibaya kwa vijana kwa kisingizio cha ajira,baadhi ya viongozi hususani wa kisiasa hutumia nafasi zao kuwashawishi kwa kuahidi ahadi zisizotekelezeka sasa mnapaswa kuyatafakari vizuri na kuyapima yale mnayoambiwa"alisema Ayoub.

Aidha Mhe Mhe Ayoub amewasistiza washiriki wa mafunzo hayo kuyatumia vyema taaluma waliyopatiwa kwa kuwaelemisha vijana wenzao katika maeneo wanayotoka ili kuweza kujikomboa kiuchumi.

"Ni tumie fursa hii kuwaomba sana mafunzo mliyopatiwa kwa muda siku mbili mkayatumie vyema kwa kuwaelimisha vijana wenzenu ili nao kwanza wajitambue lakini pia wawe wazalendo na nchi yao hatimae sasa nae waweze kuleta matokeo mazuri katika shughuli za kijamii"alieleza Ayoub.

Katika hatua nyengine Mkuu wa Mkoa ameipongeza Taasisi ya PYDOZ kwa kuaandaa mafunzo ya kuwabadili tabia na kuwawezesha vijana katika ujasiriliamali na kuwajengea mazingira bora ya maisha ya baadae.

Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya PYDOZ Salmin Shukuru Botea amesema taasisi yake itaendelea kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana wa kujitambua na ujasirimali ili waweze kujitegemea na kujitegemea na kuweza kuanzisha miradi yao na kujiimarisha kiuchumi.

"Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa uongozi wa taasisi wetu umefanya tasmini ya kutosha na kuona vijana wengi wamekuwa hawana muamko wa kujishughulisha na kazi za kujiajiri na kutaka kuajiriwa na wengine kukosa muelekeo wa maisha yao ya baadae na ndio maana tukaamua kwa makusudi kuanzisha mafunzo haya kwa vijana wenzetu"

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameelezea kunufaika na mafunzo hayo ya siku mbili ambayo yamewaongezea upeo na kuwapa mwanga wa kujitambua na kuweza kujiamini na kuweza kufanya maamuzi sahihi kwa shughuli wanazotaka kuzianzisha"

"Ki ukweli mafunzo haya yametujengea uwezo wa kujiamini na kikubwa kujitambua wengi wetu tupo katika masomo ya elimu ya juu( vyuo vikuu) lakini mafunzo tuliopewa siku mbili hizi tumejiona kuwa tofauti na ziku zilizopita,mafunzo yametupa mwanga na muelekeo wa mafanikio wa maisha yetu ya baadae"alisema mmoja ya washiki wa mafunzo hayo.

Mafunzo hayo ya siku mbili ya kuwabadili tabia na mitazamo hasi kwa vijana yameandaliwa na taasisi ya PYDOS mada mbali mbali zimewasilishwa ikiwemo kujengewa uwezo katika masuala ya ujasiriamali.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: