Rais wa Afrika Kusini, Matamela Cyril Ramaphosa ameipongeza Tanzania kwa kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi wa wastani wa asilimia 7 kwa mwaka na kubainisha kuwa hiyo ni fursa muhimu ya kuhakikisha Tanzania na Afrika Kusini zinakuza zaidi ushirikiano wa kiuchumi kwa manufaa ya pande zote mbili.

Ramaphosa amesema hayo leo tarehe 15 Agosti, 2019 katika Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima yake na Rais Dkt. John Magufuli na kufanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kuhimiza kukuza uhusiano wa kiuchumi, Ramaphosa amesema Tanzania na Afrika Kusini ambazo zinauhusiano wa kirafiki, kihistoria na kidugu zinayo changamoto ya kuhakikisha zinaliwezesha na kulitumia vizuri kundi kubwa la vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa, kwa kuhakikisha sekta binafsi inakuzwa na hivyo kuiwezesha kuajiri vijana wengi.

Ametolea mfano wa hatua zilizochukuliwa na uongozi wake za kuanzisha mpango wa kutoa vivutio kwa kampuni binafsi zinazotoa fursa kwa vijana kufanya kazi ikiwemo kuzipunguzia kodi na kubainisha kuwa mpango huo umesaidia kuwapa fursa vijana takribani 100,000 katika kipindi kifupi, ambapo wanapata fursa ya kujifunza ujuzi mbalimbali na kujenga uwezo wa kufanya shughuli za uzalishaji mali.

Ramaphosa amemponge za Magufuli kwa jitihada mbalimbali za kukuza uchumi wa Tanzania anazozifanya na amesema licha ya kumuunga mkono katika kipindi cha Uenyekiti wake wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) atakachokianza tarehe 17 Agosti, 2019 anaamini jitihada hizo pia ataziweka katika SADC.

Kwa upande wake, Rais Magufuli amemshukuru Rais Ramaphosa kwa dhamira yake ya kuendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Afrika Kusini hususani katika uchumi na amempongeza kwa mpango wake wa kusaidia vijana ujulikanao kwa jina la YES (Youth Employment Service) ambao ameahidi kuwa Serikali itaufanyia kazi ili kuona namna ya kuutekeleza hapa Tanzania.
.
Ramaphosa amesisitiza kuwa kwa hivi sasa Afrika ndio Bara lenye uchumi unaokua vizuri na linazo fursa nyingi za uchumi ikilinganishwa na Mabaramengine, hivyo ni wakati wake sasa kuchangamka na kujiimarisha.
Ijumaa (Tarehe 16 Agosti, 2019), Rais Ramaphosa ataendelea na ziara yake hapa nchini kwa kutembelea kambi ya wapigania uhuruwa Afrika Kusini iliyopo Mazimbu Mkoani Morogoro.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: