JESHI la Polisi mkoa wa Arusha,limesema kuwa litawafukuza askari wa jeshi hilo pamoja na maafisa wake bila kujali cheo chake ikiwa watabainika kuomba rushwa kutoka kwa madereva wa magari ya waongoza watalii pamoja na wamiliki wa makampuni hayo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha,Jonathan Shana ameyasema hayo kwenye kikao cha wadau wa utalii mkoa wa Arusha kilichofanyika kwenye hotel ya Gran Melia, jijini Arusha.kilichokuwa kikijadili changamoto zilizopo kwenye sekta hiyo.Akitoa salamu zake kwenye kikao hicho kilichoongozwa na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Costantini Kanyasu, Kamanda Shana amesema amepokea malalamiko ya baadhi ya askari kupokea rushwa .

Amesema kuwa ikithibitika askari ameomba rushwa kutoka kwa wamiliki wa makampuni ya waongoza utalii au madereva wa magari hayo atawafukuza mara moja na endapo kama atakuwa ni polisi mwenye nyota ataomba kibali kwa mamlaka husika cha kumfukuza afisa huyo.

Wakichangia kwenye kikao hicho wadau wamelalamikia uamuzi wa kiwanja cha kimataifa cha ndege cha Kilimanjaro, KIA, kuwalazimisha watalii kulipia malipo yao kupitia Control namb kwenye benki zilizopo nje ya uwanja huo.

Mwenyekiti wa Chama cha makampuni ya waongoza watalii, TATO, Wilbad Chambulo, amesema wageni wanapata usumbufu unaowalazimisha kutoka nje ya uwanja kwenda kulipia kwenye benki zilizoko nje ya uwanja huo halafu ndipo warejee tena uwanjani na kuiomba serikali kuboresha mfumo huo kwa kuweka benki ndani ya uwanja ili kuondoa usumbufu.

Kwa upande wake benki ya NMB imesema kuwa kuanzia Augosti 15 imesema tayari imepata meza na kuhamishia shughuli zake ndani ya uwanja huo na hivyo kuwaondolea usumbufu wageni.

Kwa upande wake Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Costantini Kanyasu,amesema Augosti 22 na 23 Wizara itafungua utalii nyanda za juu kusini mkoani Iringa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: