Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu ,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa,akizungumza na wajumbe  wakati wa  kufungua Kikao cha Baraza Kuu la wanawake Tanzania (UWT) kwa Mkoa wa Dodoma upande wa kushoto ni Mwenyekiti wa UWT mkoa Neema Majule.
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu ,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa akiwasili katika ukumbi wa CCM Mkoa Dodoma kwa ajili ya kufungua Kikao cha Baraza Kuu la wanawake Tanzania (UWT) kwa Mkoa wa Dodoma

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa amesema watu wanaombeza na kupinga jitihada kubwa zinazofanywa na Rais Dk John Magufuli watakuwa wanapingana na Mungu Mwenyewe.

Mhe Ikupa amesema hayo jijini Dodoma wakati akifunga kikao cha Baraza kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania [UWT]Kwa mkoa wa Dodoma.

Amesema mambo Mengi yaliyokuwa kwenye ilani ya Uchaguzi mkuu mwaka 2015 kwa Chama Cha Mapinduzi yametekelezwa na kubainisha kuwa mtu ambaye hajaguswa na jitihada za Rais Magufuli atakuwa Muongo.

Aidha ametaja nyanja ambazo Serikali ya awamu ya Tano imetekeleza ikiwa ni pamoja na kupambana na Dawa za kulevya ambazo zilikuwa zikipoteza vijana na kurudisha nyuma uchumi wa nchi uimarishaji wa miundombinu na umeme, barabara, reli na usafiri wa anga pamoja na uwezeshaji wa Mikopo kwa makundi maalum ikiwa ni pamoja na vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.

Hata hivyo ,Naibu Waziri huyo amechangia Jumla ya mabati 10 yenye thamani ya Tsh.360,000 Kwa UWT Dodoma kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Elimu huku jumla ya Tsh.milioni moja ,laki nane na hamsini elfu zikichangiwa kwenye harambee ya baraza hilo.

Awali akizungumza katika kikao hicho,mwenyekiti wa UWT mkoa Neema Majule amesema tangu wanaingia madarakani waliahidi mambo matatu ikiwemo kujenga UWT yenye upendo,umoja na mshikamano na kupitia mikutano mbalimbali tuliyoifanya hilo wamefanikiwa.

“Kwa sasa tumebaini na kushughulikia upatikanaji wa viwanja vya uwekezaji,na hili tumelifanya kila wilaya nia yetu tujitegemee na tusiwe tegemezi,”alisema mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake mjumbe wa Baraza kuu Taifa UWT,Chiku Mugo amempongeza Naibu Waziri Ikupa Kwa Mchango huo huku akiwapongeza wadau wengine kwa kuendelea kuiunga UWT Katika kufanikisha miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: