NA HERI SHABAN
NAIBU Waziri wa Tawala  za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mwita Waitara ameiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ikusanye mapato ili waweze kupata fedha za kutosha zikasimamie  miradi ya maendeleo.

Waitara aliyasema hayo Dar es Salaam jana, katika ziara yake endelevu manispaa ya Ilala kukagua miradi ya ya maendeleo katika sekta ya elimu.

"Nawaomba viongozi wa halmashauri muongeze kasi katika kukusanya kodi ili fedha zipatikane kwa ajili ya kusimamia miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi kwa wakati na watendaji msimamie vizuri miradi yenu "alisema Waitara

Waitara alisema mapato ambayo yanakusanywa na halmashauri hiyo shilingi bilioni 52 kwa mwaka kodi zikiwekwa katika utaratibu mzuri zitatatua kero katika huduma za jamii.

Alisema dhumuni la ziara yake kuangalia fedha ya serikali shilingi milioni 425 zilielekezwa katika sekta ya elimu kama zimefanya kazi iliyokusudiwa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa  .

Aliwapongeza manispaa ya Ilala kwa kukamilisha ujenzi wa madarasa ya wanafunzi katika sehemu ambayo fedha imeelekezwa.

Wakati huo huo ameigiza halmashauri ya Ilala  iweke Wataalam wa kutosha katika kusimamia  ujenzi wa shule ya Msingi mpya  ya Gulukwa lala   na shule hiyo ijengwe vizuri watoto waje kusoma.

Aidha alishauri katika ujenzi wa shule hiyo ya Gulukwa lala wawape wazawa ajira ili waweze kujiongezea  kipato .

Pia alisema Manispaa hiyo imeajili walimu 4500 wapya nchi nzima imeajili walimu 22000 hivyo changamoto za walimu mashuleni zitapungua


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala Elizabeth Thomas alisema eneo la mradi shule ya Msingi Guluukwa lala hekari tatu itajengwa vyumba 23 kila kitu kitakuwepo ikiwemo ofisi za walimu.


Kwa upande wake Msimamizi wa mradi wa shule ya Msingi Gulukwa lala Saimoni Mndeme alisema  ujenzi huo utachukua siku 60 kukamilika kwake.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: