Saturday, 10 August 2019

MAJALIWA AFUNGUA NYUMBA ZA MAKAZI YA POLISI MJINI SHINYANGA.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuzindua nyumba 10 za makazi ya Askari Polisi mjini Shinyanga, Agosti 9, 2019. Majaliwa Agosti 9, 2019 aliwakabidhi funguo za nyumba  Askari Polisi 10 baada ya kufungua nyumba za makazi yao mjini Shinyanga. Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akimkabidhi, Koplo Tegemea Masatu ufungua wa nyumba aliyopangiwa kuishi. Katikati ni Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyanga, ACP Richard Abwao. Majaliwa akikagua moja kati ya nyumba 10 za Askari Polisi alizozifungua na kukabidhi funguo kwa Askari waliopangiwa kuishi katika nyumba hizo mjini Shinyanga, Agosti 9, 2019.  Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellak na wa tatu kulia ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga,  ACP Richard Abwao.Majaliwa akikagua moja kati ya nyumba 10 za Askari Polisi alizozifungua na kukabidhi funguo kwa Askari waliopangiwa kuishi katika nyumba hizo mjini Shinyanga, Agosti 9, 2019.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellak na wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mbaneko.Majaliwa akipanda mti baada ya kufungua nyumba za makazi ya Askari Polisi mjini Shinyanga, Agosti 9, 2019. Kulia ni Waziri  wa Kilimo, Japhet Hasunga na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zaib Tellak. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)