Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam kupitia kwa  Lazaro Mambosasa  limesema limejipanga kuimarisha ulinzi wakati wa Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika jijini Dar es Salaam.

 Aidha katika kipindi hiki cha mkutano wa SADC Jeshi la polisi kanda maalum Dar es Salaam linapiga marufuku mambo yafuatayo;

1.Marufuku pikipiki (Bodaboda )zote kuingia katikati ya Jiji kuanzia tarehe 06 August hadi 18 August, 2019 kutokana na sababu ya baadhi ya bodaboda kujihusisha na vitendo vya uhalifu

2. Marufuku kuweka taa za vimulimuli au za rangi rangi, taa zenye mwanga mkali (spot light) na kufunga ving’ora kwenye Magari ya kiraia au watu binafsi na pikipiki zote za kiraia

3. Marufuku kuingilia misafara ya wageni, wananchi wanatakiwa kuwa wavumilivu kipindi hiki cha ugeni mkubwa wa kimataifa.

“Katika kipindi hiki cha mkutano wa SADC Jeshi la polisi kanda maalum DSM linapiga marufuku pikipiki (Bodaboda )zote kuingia/kufika maeno yote ya katikati ya Jiji kuanzia August 06 hadi August 18,2019 kutokana baadhi ya bodaboda kujihusisha na vitendo vya uhalifu.

“Polisi inapiga marufuku kuweka taa za vimulimuli au za rangi rangi, taa zenye mwanga mkali (spot light) na kufunga ving’ora kwenye magari ya kiraia au watu binafsi na pikipiki za kiraia, isipokuwa magari yanayotoa huduma za dharura tu na ya makampuni binafsi ya ulinzi” Amesema Mambosasa
Share To:

msumbanews

Post A Comment: