Na Ferdinand  Shayo,Arusha.
Chama cha Mapinduzi  Wilaya ya Karatu kimefanya ziara yake na kubaini miradi iliyosimama bila kutekelezwa kwa muda na kusababisha adha kwa wananchi ikiwemo mradi wa zahanati ya kijiji cha ambayo imesimama kwa miaka 12 tangu ilipojengwa bila kukamilika .
Kamati ya Siasa ya Wilaya ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Karatu  Lucian Akonay ,Katibu wa Chama Shaban Mrisho,Katibu Mwenezi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi.Theresia Mahongo.
Mwenyekiti wa Ccm wilaya ya Karatu Lucian Akonay  ameitaka serikali kuharakisha kumalizia zahanati hiyo kwani kukosekana kwa huduma hiyo kunawanyima haki ya matibabu wananchi hivyo amewaonya watendaji wanaolega lega kuchukua hatua kukamilisha mradi huo.
Aidha amewataka Watendaji kukamilisha mradi huo kabla ya mwaka huu kuisha ili wananchi waweze kupata huduma kwa karibu.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu Waziri Morris  wamesema kuwa juhudi za kumalizia kituo hicho zinaendelea ili kwa mwaka wa fedha 2019/20 waweze kukamilisha wakishirikiana na nguvu za wananchi.
Hata hivyo Katibu wa Ccm wilaya hiyo Shaban Mrisho amemuomba Raisi Magufuli kuwachukulia hatua waliofanya ufisadi na kukifilisi kiwanda cha maziwa cha Ayalabe   kwani kwa kufanya hivyo wanahujuma juhudi za kufukia uchumi wa viwanda na uchumi wa kati.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: