Friday, 9 August 2019

Bonah awataka wana ccm kushikama ili kushika dolaNA HERI SHAABAN(Kiwalani)

MBUNGE wa Segerea (CCM)Bonah Ladslaus amewataka wana ccm wa Kiwalani kushikamana kuwa wamoja katika kukipigania chama cha Mapinduzi na kuakikisha kinashika dola uchaguzi wa Serikali za Mitaa.Bonah aliyasema hayo Dar es Salaam leo wakati wa kuzungumza na viongozi wa chama wa kata ya Kiwalani wakati wa ziara yake ya kuwamashisha kushiriki katika uchaguzi wa Serikali Mitaa Mwezi Novemba mwaka huu.

"Nawaomba wana CCM wenzangu wa Kiwalani tunaelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa nawaomba tushirikiane katika kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi na kuakikisha ccm inashinda kwa kishindo uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa Rais" alisema Bonah.

Bonah aliwataka wana ccm kuwa wamoja  na kujenga mahusiano na wananchi wao wanaowazunguka katika kushirikiana katika shughuli za maendeleo.

Aliwataka viongozi wa chama kuwa karibu na wanachi wao na kuwashirikisha katika shughuli za maendeleo .

Kwa upande wake Mwenezi wa Wilaya ya Ilala Saidi Sidde aliwataka viongozi wa  ccm wa wilaya hiyo kutenga kila mwisho wa mwezi kufanya shughuli za kijamii ikiwemo usafi katika maeneo yao.

Sidde alisema kila kiongozi wa Chama ana wajibu wa kutekekeza agizo la serikali  ya awamu ya tano kufanya usafi kila mwisho wa mwezi.

Pia aliagiza kila kata zilizopo manispaa ya Ilala kiongozi wa chama ana wajibu kufatilia kujua fedha za miradi ya maendeleo.

MWISHO
09/08/2019