Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza kuongeza muda wa kuomba mkopo kwa njia ya mtandao kwa siku saba hadi Ijumaa, Agosti 23, 2019 ili kuwapa fursa waombaji ambao hawajakamilisha maombi yao kutumia muda ulioongezwa kufanya hivyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema jijini Dar es salaam leo (Alhamisi, Agosti 15, 2019) kuwa HESLB ilianza kupokea maombi ya mkopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020 tarehe 1 Julai mwaka huu na tarehe ya mwisho ilipaswa kuwa leo, Agosti 15, 2019.

Kwa mujibu wa Badru, HESLB imepokea maombi kutoka kwa baadhi ya waombaji mikopo ambao hawajakamilisha maombi yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa nyaraka muhimu.

“Ingawa hadi leo asubuhi (Agosti 15, 2019) tumeshapokea maombi zaidi 74,821 yaliyokamilika kwa njia ya mtandao, tumepokea pia maombi kutoka kwa wateja wetu wakitaka kuongezewa muda ili wakamilishe nyaraka muhimu kama nakala za vyeti vya vifo vya wazazi wao, barua kutoka kwa wadhamini wao na nyaraka nyinginezo … tumewasikiliza na kuongeza muda,” amesema Badru.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amewataka waombaji mkopo ambao hawajakamilisha maombi yao kutumia muda ulioongezwa kukamilisha maombi yao kwa kuwa HESLB haitaongeza muda zaidi baada ya tarehe 23 Agosti mwaka huu.

“Tunasihi waombaji wetu watumie muda huu ulioongezwa kukamilisha maombi yao kwa kuwa hatutaongeza tena. Baada ya Agosti 23, tutaanza kufanya uchambuzi wa maombi tuliyopokea ili tuwapangie mikopo wenye sifa kwa wakati na tupeleke fedha za mikopo vyuoni kabla vyuo havijafunguliwa,” amesema Badru na kuongeza:

“Tunawaomba wadau wetu kama Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar na Shirika la Posta Tanzania (TPC) kuendelea kuwahudumia wanafunzi katika kipindi hicho,” amesema.

Katika kipindi kilicho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: