Wednesday, 24 July 2019

Waziri Ndalichako Awapongeza walimu wa Bwiru


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Joyce Ndalichako,amekagua ukarabati katika shule ya sekondari ya wasichana Bwiru ukarabati huo umefanywa na Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA).
Pamoja na hayo amewataka wanafunzi kuzidisha bidii katika masomo

Mhe.Ndalichako pia amewapongeza walimu wa shule hiyo kwa juhudi walizozifanya katika kuhakikisha kuwa wanafuta daraja 0 katika matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka 2019.Pia amewaomba TEA kujenga bweni la wasichana ili kuondoa msongamano wa wanafunzi katika mabweni.

Shule ya sekondari ya wasichana Bwiru ilifanyiwa ukarabati mkubwa wa majengo na miundombinu chini ya mamlaka ya Elimu Tanzania.Mradi huu ulianza kutekelezwa Februari 2018 na kukamilika Septemba 2018 ambapo jumla ya kiasi cha Tsh.974,976,472.91 zilitolewa kwa ajili ya kukarabati mabweni,madarasa,vyoo,maabara,jiko na bwalo,ukumbi ba jengo la utawala na mgahawa.

Mradi huu umetekelezwa kupitia utaratibu wa Force akaunti na kusimamiwa na wataalam washauri toka chuo kikuu cha sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

No comments:

Post a Comment