Tuesday, 16 July 2019

WATAALAMU WA AFYA TOENI ELIMU SAHIHI YA AFYA YA UZAZI KWA WANAWAKE, KUTOKIMBILIA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJIMkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Gabliel Daqarro leo Jully 16 2019 amezindua rasmi kampeni ya ya Afya ya mama na mtoto yenye jina la "JIONGEZE TUEAVUSHE SALAMA" lengo kuu likiwa ni kutokomeza vifo vya mama mjamzito pamoja na mtoto.

Awali kampeni hii ya JIONGEZE TUWAVUSHE  SALAMA ilizinduliwa rasmi na makamu wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samiha Hassan Suluu June 6 2018 na badae ilizinduliwa kimkoa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo April 16 mwaka.

Katika uzinduzi huo wa Afya ya mama na mtoto Dc Daqarro ameonya vikali juu ya uzembe wa watumishi wa serikali katika vituo vya Afya katika jiji la Arusha kwa kuwa wazembe wakati wa hutoaji wa huduma kwa wanawake wajawazito na kutoa maelekezo kwa uongozi wa Afya jiji la Arusha kuweza kutoa elimu ya mwanamke kujifungua kwa njia ya kawaida na kuacha kujifungua kwa upasuaji.

"Mpaka sasa wasichana wengi wanao anza uzazi huwa hawapendi kupata uchingu wa  uzazi wao kazi yao kubwa wakiona siku za kujifungua zimefika anaenda kwa dactari anamwambia chana hapa." alisema  Dc Daqarro.

Aidha pia Daqarro aliwataka wataalamu wa Afya wote kujitagidi kadri ya ujuzi wao ili kuondoa vifo vya mama na mtoto kaktika jiji la Arusha,viongozi wa dini kukemea mimba za utoto na kwa wakuu wa mila kuacha imani potofu kwani kwa kila mmoja kufanya majukumu yake kutasaidia zaidi kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Nae kwa upande wake Dactari mkuu wa mkoa wa Arusha Welson Sichalwe ameeleza kuwa kwa mwaka jana vifo vya mama na mtoto vilivyo tokea ni 116 katika uzazi hai 7000 na huku watoto 10 katika uzazi hai 1000 na kueleza yote haya yanatokea kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo lishe duni.

Pia Dr Welesnon amebainisha kuwa katika awamu hii ya tano ya Docta John Pombe Magufuli imeendelea kupamba na kuboresha secta ya Afya na kufanya mkoa wa Arusha kuwa na wastani wa akiba ya azina ya madawa kwa 97% ya dawa zote na kuwa na viyuo vya Afya 12 na zahanati 1 hivi vyote vimeghalimua zaidi ya bilioni 16 za kitanzania.

No comments:

Post a Comment