Wananchi wa Kitongoji cha Kaugeri Kata ya Mwaru katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wakimlaki Mbunge wao Elibariki Kingu baada ya kuwasili kwa ajili ya kufanya mikutano ya hadhara kwenye kata hiyo jana.
Wananchi wa Kitongoji cha Kaugeri Kata ya Mwaru wakiwa wamembeba mbunge wao.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi,  Elibariki Kingu akipata maelezo kutoka kwa Diwani wa Kata ya Mwaru, Iddi Makangale alipo kuwa akikagua ujenzi wa Zahanati ya Kitongoji cha Mlandala.
 Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi,  Elibariki Kingu akizunfumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mlandala.
 Diwani wa Kata ya Mwaru, Iddi Makangale akizungumza na Wananchi wa kitongoji cha Mlandala katika mkutano wa mbunge huyo.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi,  Elibariki Kingu akiwahutubia  Wananchi wa kitongoji cha Mlandala
 Mkutano ukiendelea kitongoji cha Mlandala.
 Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi,  Elibariki Kingu akiwa katika picha  na viongozi pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kaugeri baada ya kukagua ujenzi wa shule hiyo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kaugeri wakitoa burudani kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
 
WANANCHI wa Kitongoji cha Kaugeri Kata ya Mwaru katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wameshindwa kujizuia furaha yao na kujikuta wakimbeba na kusukuma gari la Mbunge wao Elibariki Kingu kutokana na jitihada zake za kuwapelekea miradi ya maendeleo.
 
Wakiongea kwa nyakati tofauti jana kwenye mikutano ya hadhara aliyoandaa mbunge huyo katika vitongoji vya Kaugeri na Mlandala walisema haijawahi kutokea tangu vianzishwe vijiji hivyo kwa kupata maendeleo makubwa katika kipindi cha miaka minne tangu mbunge huyo aingie madarakani.
 
Akizungumza katika mkutano huo mmoja wa wananchi wa kitongoji cha Kaugeri aliyejitambulisha kwa jina moja la Maganga  alisema haijawahi tokea mbunge wa mfano kama Kingu.
 
” Mbunge huyu hana wa kumlinganisha naye amejitahidi sana kutuletea maendeleo katika Kata yetu yenye vitongoji vitano vya Kaugeri, Mdughuyu, Mlandala, Mpugizi na Mwaru.
 
Alisema katika vitongoji hivyo ameweza kujenga shule, zahanati na sasa amewaletea mradi mkubwa wa maji ambao utasambaza maji kwenye vitongoji vyote vya kata hiyo.
 
Diwani wa Kata hiyo Iddi Makangale alisema tangu miaka 50 iliyopita hakujawahi kutokea Mbunge kama Kingu kwani kazi iliyofanywa na Rais John Magufuli na Mbunge huyo kwa kushirikiana na wananchi imewarahisishia upatikanaji wa kupata kura nyingi katika uchaguzi mkuu kwa chama chao cha Mapinduzi (CCM).
 
” Kwa kazi hii kubwa iliyofanyika hatuna wasiwasi CCM itapata ushindi mnono ambao haujawahi kupatikana katika uchaguzi wowote tuliowahi kuufanya” alisema Makangale.
 
Akizungumza katika mkutano huo Kingu aliwashukuru wananchi hao na kuwaambia maendeleo hayo wanayapata baada ya Rais John Magufuli kuwabana mafisadi na matumizi mabaya ya fedha na kuzielekeza kwa wananchi wanyonge kwa kuwapelekea miradi ya maendeleo.
 
Alisema haijawahi kutokea kwa kipindi chote kilicho pita katika jimbo hilo kufanyika kwa miradi mingi kiasi hicho ikiwemo miradi mikubwa ya maji 22 huku mchakato wa kupata umeme wa REA ukiendelea.
 
Kingu aliwataka wananchi wa kata hiyo kuacha majungu badala yake wafanye kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo.
 
Katika hatua nyingine Kingu anatarajia kuitisha mkutano mkubwa wenye lengo la upigaji kura ya kuwabaini wahalifu wa mauaji ya watu katika Kata ya Mwaru kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: