Wednesday, 17 July 2019

Waliofariki kwa kuporomokewa na ghorofa wafikia 14Idadi ya vifo kutokana na kuporomoka kwa jengo moja lenye ghorofa nne mjini Mumbai nchini India imeongezeka hadi 14.

Polisi hapo jana walisema watu wengi bado wanahofiwa kuwa wamekwama chini ya vifusi hivyo huku mashine za uokoaji na vifaa zikishindwa kufikia eneo hilo kutokana na njia nyembamba na kuna uwezekano idadi hiyo itaongezeka.

Timu tatu kutoka kwa Jeshi la Taifa la Maafa zinaendelea katika shughuli za uokoaji. Wakazi wa majengo yaliyo karibu pia wamehamishwa kwenye shule iliyo karibu kama hatua za tahadhari.

No comments:

Post a Comment