Saturday, 13 July 2019

VIJANA WA UVCCM ARUSHA WATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SIO BORA KIONGOZI

 Picha ikionyesha wagombea  wanafasi  ya uwenyekiti wa vijana  mkoa wa Arusha wakiwa katika  picha ya pamoja kabla ya uchaguzi kuanza.
 Picha baadhi ya vijana wa Uvccm wakiwa ndani ya ukumbi kabla ya uchaguzi kuanza
Picha baadhi ya vijana wa Uvccm wakiwa ndani ya ukumbi kabla ya uchaguzi kuanza

Na  Woinde Shizza,Arusha

Katika  kupata viongozi wanaofaa Vijana wametakiwa kuchagua viongozi ambao wanaakili ,busara ,hekima,uwelevu  pamoja na wale ambao wataweza kuwaletea maendeleo katika kipindi chake cha uongozi.

Hayo yamebainishwa na mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa vijana Jafari Mghamba wakati akiongea  na vijana leo katika mkutano mkuu wa maalum wa uchaguzi wa mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoa wa Arusha (UVCCM) ambapo amewataka  vijana kuacha kuchagua viongozi kwa miamko ,pamoja na ushabiki kwani kufanya hivyo ndio kunapelekea kupata viongozi ambao hawawezi kuleta maendeleo wala mabadiliko yoyote katika jamii.

Alisema kuwa wanatakiwa kuchagua viongozi ambao wataleta twaswira nzuri na maendeleo katika chama  cha mapinduzi  ,kwa kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi.

Aidha aliwataka wananchi kuwachagua viongozi bora kwa ajili ya maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla wake ,alibainisha kuwa nivizuri tusiwachague viongozi kwa majaribio wala kwa ushabiki bali wanatakiwa kuchagua viongozi wananaofaa na tuliowazoea na tunaowajua vizuri tabia na mienendo yao.

"vijana wa UVCCM msifanye makosa ya kudanyanywa na kuchagua viongozi wasiofaa na ambao hatuwafahamu vizuri mimi naamini kiongozi mtakae mchagua leo ni bora na sio bora kiongozi "alisema msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni mjumbe wa halmashauri kuu CCM taifa Livingstone Lusinde.
 
Alimalizia kwakuwatakia uchaguzi mwema ambapo alisema anaamini amani itaendelea kutawala katika umoja huu wa vijana mkoa wa Arusha  huku akisisitiza atasimamia uchaguzi huu kwa kufuata sheria inayoongozwa na ilani ya CCM. 

Wagombea wanaogombea nafasi ya uwenyekiti wa vijana wa mkoa wa Arusha ni pamoja na Rovet Philimon,Omary Lumato pamoja na Suleman Msuya.

No comments:

Post a Comment