MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akizungumza wakati wa Fainali ya Ligi ya Adadi Cup iliyofikia tamati mwishoni mwa wiki ambayo huchezwa Jimbo nzima lengo likiwa kuinua vipaji vya wachezaji wachanga wilayani humo kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha soka wilaya ya Muheza (MDFA) Yusuph Salim alimarufu Maji Safi.
 Mwenyekiti wa Chama cha soka wilaya ya Muheza (MDFA) Yusuph Salim alimarufu Maji Safi akizungumza wakati wa fainali hiyo
 MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kulia akimkabidhi kombe la Ubingwa wa Kombe la Adadi Cup nahoda wa timu ya Mjesani FC ambao ni mabingwa wapya wa Kombe hilo
 MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akkiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya Mjesani FC ambao ni mabingwa wa Kombe la Adadi Cup
 MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akisalimiana na timu zinazoshiriki fainali ya Kombe hilo
 MBUNGE wa Jimbo la Muheza CCM Balozi Adadi Rajabu katika akifuatilia fainali ya Adadi Cup

NA MWANDISHI WETU, MUHEZA

TIMU ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars”imeelezwa kwamba inaweza kufanya makubwa kwenye michuano ya Chan na kuweza kung’ara kutokana kikosi chake kuimarika kwenye Mashindano ya Afcon yaliyomalizika hivi karibuni.

Kwani hilo linatokana na kuwepo kwa wachezaji wazuri wenye uwezo kwenye kikosi cha timu hiyo ambao wanaweza kukabiliana na chochote hatua ambayo inawapa matumaini makubwa.

Hayo yalisemwa na Mbunge wa Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajabu wakati akizungumza katika fainali ya Ligi ya Adadi Cup iliyoianzisha kwenye Jimbo nzima ikiwa ni mpango mkakati wa kukuza soka na kuibua vipaji.

Katika mashindano hayo timu ya Mjesani ya Kata ya pande iliweza kutawadhwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi hiyo baada ya kuibamiza mabao 7-6 City Centre ya Kicheba na kukabidhiwa Kombe,Laki tano,Ng’ombe,Jezi na Mpira mmoja,mshindi wa pili ni Kicheba City Center laki tatu,mbuzi na jezi na mshindi wa tatu mashabiki wa Simba wamepata laki moja na jezi.

Alisema kwamba ligi hiyo inachezwa kwenye Tarafa nne wilayani humo lengo likiwa ni kuibua na kukuza vipaji vya wachezaji wachanga ambao baadae wanaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye soka.

Aidha pia alisema kwamba ligi hiyo imesaidia kuibua vipaji vya wachezaji vijana ambao ndio baadae wanaweza kuisaidia timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” katika miaka ijayo hapa nchini.

“Kikubwa tuangalie namna ya kukuza vipaji huku akitaka uteuzi wa wachezani wa timu ya Taifa uangalie kwenye michezo kuanzia ngazi ya wilaya kuendelea juu ambako kunaweza kupatikana wachezaji wazuri”Alisema.

Mbunge huyo alisema wachezaji wa timu ya Taifa ambao wapo walishiriki kwenye mashindano ya Afcon anaamini wanaweza kuleta mapinduzi makubwa kwenye michuano ya Chan kutokana na kundi ambalo wamepangwa nalo

Naye kwa upande wake kwenye michezo kuna Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wilaya ya Muheza (MDFA) Yusuph Salim alimaarufu Maji Safi alisema mashindano hayo yalishirikisha timu 16.

Alisema mashindano hayo yameweza kufanikiwa kuibua vipaji vya wachezaji wa soka wilayani humo huku akiwataka vilabu vinavyoshiriki ligi mbalimbali ikiwemo Ligi kuu kupita wakati inapoanza ili kusaka wachezaji.

Katibu huyo alisema uanzishwaji wa Ligi hiyo umesaidia kuinua soka wilayani humo huku wakimshukuru Mbunge wa Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajabu ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha michezo inaimarika wilayani humo.

mwisho
Share To:

Post A Comment: