Muonekano wa Bwalo la Wanafunzi wenye mahitaji maalumu linalojengwa katika Shule ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Chuo cha Ualimu Patandi, Arumeru mkoani Arusha
Muonekano wa Jengo la Utawala la Shule ya Wanafunzi wenye mahitaji maalumu inayojengwa katika Chuo cha Ualimu Patandi.
 
Zaidi ya shilingi bilion 2.8 zimetolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa shule ya secondary ya elimu maalumu katika eneo la chuo cha Patandi kilichopo Tengeru wilaya ya Arumeru mkoani Arusha

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya miundombinu wilayani Arumeru Mkuu wa wilaya hiyo Mh, Jery Muro amesema kuwa fursa hiyo ni ya kwanza hapa nchini ambapo italeta manufaa kwa watu wenye mahitaji maalumu

Amesema kuwa licha ya kusaidia kitaleta kielelezo cha kuhakikisha watoto wenye ulemavu watapewa mtazamo mpya wa elimu kwa kuokoa watoto wenye changamoto na mahitaji maalumu kutoka sehemu mbalimbali 

Aidha ameseama kila mwezi serikali inatoa bilioni 23 kwa wastani kwa ajili ya ujenzi wa elimu na kugharamia sera ya elimu bure hapa nchini 

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya mahitaji maalumu Patandi Mwl. Janeth Molel ameipongeza serikali kwa juhudi kubwa za kuwajali watu wenye mahitaji maalumu hasa kupitia elimu kwani hii itasaidia kupunguza ongezeko la watoto wa mtaani na hatiamye kufikia malengo ya Tanzania ya viwanda

Amsesema kuwa,kwa sasa yamekamilika madarasa manane 8 na itachukua wanafunzi wenye mahitaji maalumu ambapo tayari wameshapata waalimu 5 kwa ajili ya kuanza kutoa elimu hiyo ambayo itakuwa shule ya mfano hapa Tanzania.

Amewataka wazazi kutowaficha watoto wao wenye ulemavu bali watumie fursa iliyojitokeza katika kuhakikisha wanawapatia elimu ambayo itawasaidia katika kujenga msingi mzuri wa maisha

Kwa upande wake mbunge wa Arumereru Mashariki John, Danielson Palanjo amesema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha elimu inapewa kipaombele hasa kwa watu wenye mahitaji maalumu kwa kuwa nao wana uwezo wa kulitumikia taifa

Amesema huduma ya elimu katika ambayo imeletwa wilayani hapo, italeta manuafaa kwa jamii na kuwa mfano kwa huiduma ambazo kila mtu atazifaidi kwa kuwa itakuwa tegemezi kwa kila mwananchi

Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Meru Bw. Emanuel Mkongo amesema wao kama halmashauri bwanasubiri kukabidhiwa madarasa na pia watahakikisha kila kitu kimekamilika ili kuweza kuruhusu wanafunzi kuingia madarasani ambapo nao wana mchango mkun=bwa katika kuhakikisha wanaungana na serikali kuendeleza watu wenye mahitaji maalumu 

Hata hivyo shule hiyo itakuwa na uwezo wa kuwa na wanafunzi 120 wenye mahitaji maalumu bila ubaguzi na watapata huduma mabalimbali kulingana na uwezo wao
 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: