Baadhi ya madarasa yaliyofanyiwa ukarabati na Taasisi za Chemchem Association.
Kikao cha vikoba wananchi wa vilima vitatu kikiendekea
Madawati yametolewa na Kampuni ya Taasisi za Chemchem Association shule msingi Vilima vitatu.
Baadhi ya madarasa yaliyofanyiwa ukarabati na Taasisi za Chemchem Association ambapo kwa jumla yake yapo saba.

Hayo madawati yametolewa shule msingi Vilima vitatu, na hiyo ndio shule iliyokarabatiwa na hapo kikao cha vikoba wananchi wa vilima vitatu


Na Vero Ignatus,Arusha

Zaidi ya sh 100 milioni imepangwa  kuchangia miradi ya Maendeleo katika eneo la Jumuiya ya  hifadhi ya jamii ya Wanyamapori( JUHIBU kutoka kwa Taasisi za Chemchem Association.

Taasisi hiyo ya JUHIBU, ilianzishwa mwaka 2003 ambapi inaundwa na vijiji vya Sangawe,Mwada,Ngoley,Vilimavitatu,Minjingu,Kakoi,Olasiti,Manyara,Magala, na Maweni na ina ukubwa wa 283.

Walter Palangyo ni Afisa Maendeleo ya jamii ya Taasisi ya  Chemchem association,  amesema taasisi inachangia miradi hiyo kama sehemu ya wajibu wake kuchagia shughuli za Maendeleo ya jamii(SCR) mbali ya kodi na tozo nyingine zinazolipwa na Chemchem iliyowekeza shughuli za Utalii katika hifadhi hiyo.

Amesema  taasisi hiyo, imekamilisha  ukarabati wa majengo ya shule ya msingi vilima vitatu,ofisi mbili za walimu na sasa ipo kwenye mradi wa ujenzi wa vyoo .

"katika shule hii, tumetumia kiasi cha sh 50 milioni, ili kuhakikisha wanafunzi katika shule hii wanapata elimu bora katika mazingira mazuri kwani tayari tumewapatia  madawati 100  kwa ili kumaliza tatizo katika shule hii"alisema

Amesema taasisi  hiyo pia imetoa kiasi cha sh 5 milioni ili kusaidia Vikoba katika baadhi ya vijiji katika eneo hilo, ikiwepo vikundi vya jamii ya wabarbeig ili kuweza kuwa na miradi ya maendeleo.

"Kuna kikundi cha Wicheda na Datoga vya jamii ya Kibarbeig  ambavyo tumepatia kiasi cha sh 2.5 milioni ili kukuza mitaji yao"alisema

Alisema katika jamii hiyo, pia kumeanzishwa mradi wa maboma ya asili ambayo watalii wataweza kuwatembelea .

"Mwaka huu pia tunaendelea na mradi wa kusomesha watoto katika jamii hii, katika chuo cha wanyamapori cha Mweka na chuo cha Ufundi (VETA) naa wengine tumewalipia ada za shule ya sekondari "alisema

Amesema  pia kuna miradi ya maji, michezo na afya  katika vijiji hivyo, hasa kutokana na fedha ambazo zinatokana na la ya utalii.

MWISHO.






Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: