Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akiangalia kiti na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiangalia dawa
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali mmoja wa wagonjwa
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipanda mti

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeshusha neema kwa Wananchi wa Mkoa wa Njombe kwa kutenga kiasi cha shilingi Bilion 7.6 kwaajili ya ujenzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe ili kuboresha huduma kwa Wananchi.

Hayo yamejiri leo wakati wa zoezi la Uzinduzi wa huduma za Afya na lililoongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe iliyofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika uzinduzi huo, Waziri Ummy amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha huduma za Afya katika Mkoa wa Njombe ikiwemo kujenga jengo la wazazi la ghorofa tatu, jengo la maabara, jengo la wagonjwa mahututi na jengo la upasuaji gorofa mbili, wodi za wagonjwa gorofa tatu, nyumba za Watumishi tano, pamoja na kichomea taka.


" Tunajenga jengo la wazazi la ghorofa tatu, tunajenga jengo la jengo la maabara, tunajenga jengo la wagonjwa mahututi na jengo la upasuaji gorofa mbili, tunajenga wodi za wagonjwa gorofa tatu, tunajenga jengo la kufulia, tunajenga kichomea taka na tunajenga nyumba za watumishi tano" alisema Waziri Ummy.

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amemwagiza Mkandarasi wa Hospitali hiyo kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa majengo hayo hayo ndani ya miezi kumi ili wananchi wa Mkoa wa Njombe waanze kufaidika na huduma za Afya katika Hospitali hiyo, huku akiwatoa hofu wananchi kuwa pesa zote zipo tayari.

Mbali na hayo, Waziri Ummy mewaasa Wananchi kupambana dhidi ya magonjwa yasiyo yakuambukiza kama Kisukari, shinikizo la damu, Saratani na magonjwa ya Moyo kwa kubadilisha mtindo wa maisha ikiwamo ulaji mlo sahihi , kuacha uvutaji wa sigara na tumbaku, kuacha unywaji wa pombe kupita kiasi pamoja na kutofanya mazoezi mara kwa mara.

Aidha, Waziri Ummy ametoa with kwa vijana kujiepusha na mambo ambayo yatapelekea kipata maambukizi ya VVU, huku akiweka wazi kuwa maambukizi mapya ya VVU ni 82,000 kila mwaka nchini Tanzania, huku katika kila watu 100, watu 40 ni vijana wenye umri kati ya 15 hadi 24 umri ambao ni nguvu kazi ya taifa.

"Tunatambua kwamba kuna maambukizi makubwa ya virusi vya Ukimwi Mkoani Njombe,lazima tuzingatie kanuni za kujikinga na maambukizi ya VVU, kujizuia kufanya mapenzi kwa vijana hasa kwa wasichana ambao muda wao haijafika, pili kuwa mwaminifu kwa mwenza wako au mpenzi wako na tatu kutumia kinga" alisema Waziri Ummy

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka amewatoa hofu wananchi wa Mkoa wa Njombe kwa kuweka wazi kuwa huduma za Afya katika Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe haitoathiri utoaji huduma katika Hospitali ya Kibena iliyokuwa Hospitali ya Mkoa, ambayo kwa sasa imerudishwa chini ya Halmashauri ya Mji wa Njombe.

"Na mimi ntahakikisha wale Watumishi ambao tilikubaliana waje kwenye Hospitali hii, waje na nguo zao , vifaa vyote waviache Kibena na huduma ya Kibena iendelee, na kazi ya Hospitali hii Mhe. Ummy Mwalimu na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wataweka vifaa vyote vitakavyohitajika na huduma zitaendelea" alisema Mhe. Olesendeka

Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Mhe. Edwirn Mwanzinga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kupitia Wizara ya Afya kwa kuongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba jambo linalosaidia kuokoa kwa kiasi kikubwa maisha ya Wananjombe.

Mwisho.
Share To:

Post A Comment: