Katika kutekeleza ilani ya CCM ya 2015/2020 ibara ya 53,54,55 na vifungu vyake..

Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera  tarehe 11.07.2019 amezindua mradi wa maji katika kijiji cha Chamalendi kata ya Chamalendi Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe wilayani Mlele.

Mradi huo wenye thamani ya Tsh 402,600,000/= umeshuhudiwa na mamia ya wananchi . Mradi huu utahudumia wananchi zaidi ya 10,000 Katika kata hiyo ya chamalendi.

Ikumbukwe kuwa, lengo la serikali inayoongozwa na Rais wetu Mpendwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ni kufikisha maji mpaka kijiji cha mwamapuli na vijiji vya jirani.

Hata hivyo mkuu wa mkoa Homera aliwaomba wananchi wa Kijiji cha Chamalendi na kata hiyo kwa ujumla kuendelea kumuombea Raisi Wetu awe na afya njema aendelee kuwatumikia vyema watanzania na wanakatavi wote kwa ujumla.

Pamoja na hayo, RC Homera amempongeza waziri wa Maji Prof Makame Mnyaa Mbarawa kwa usimamizi wa karibu wa miradi ya maji mkoani Katavi na kupelekea kutekelezwa kwa asilimia zaidi ya 99%, hivyo amewaomba wananchi waendelee kumwombea afya njema Mhe *Mbarawa* pia.

Mwisho, Mkuu wa wilaya hiyo ya Mlele Mhe. Rachel Kasanda amewataka wananchi hao kuutunza Mradi huo kwa kutumia vyema fedha za michango ya watumia maji ili mabomba yakiharibika waweze kukarabati na kuongeza vioski vingine vya kuchotea maji kutoka 20 na kuongeza vingine zaidi.


Share To:

Post A Comment: