Umati wa waumii waliofurika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikhe Amri Abeid Karume Jijini Arusha kusikiliza neno la Mungu linaloendelea kuhubiriwa na Muhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Sweeden Johannes Amrizer ambapo unakwenda sambamba na maadhimisho ya mika 80 ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God Tanzania.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo akisalimia wananchi waliohudhuria katika mkutano huo wa neno la Mungu ambao ulianza rasmi siku ya Jumatano ambapo siku ya kesho ndiyo Kilele chake.
Muhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Sweeden Johannes Amrizer akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo jioni ya leo 

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema Taifa linahitaji viongozi wa dini wanaohubiri habari njema kuhusiana na Mungu kwaajili ya kuleta Amani katika Taifa na wananchi kwa ujumla.

Mhe. Gambo ameyasema hayo jioni ya leo  katika mkutano wa Injili unaoendelea katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid alipokaribishwa kusalimia waumini waliokuwepo na muhubiri wa Kimataifa Johannes Amrizer kutoka nchini Sweeden."

Amesema kuwa kesho ni kilele cha maadhimisho miaka 80 ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God Tanzania hivyo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuungana na kanisa holo la TAG kusheherekea mwambie hata mwenzio aliyeko nyumbani.aje.kusikiliza.siyo.dhambi"

Waambieni wengine waliopo nyumbani wamechelewa angalau wajitahidi wafike siku ya kesho ili waweze kupata majumuisho ya kile kilichokuwa kinaendelea uwanjani hapa kwa wiki nzima"Alisema.Gambo.

 Gambo amewahakikishia wananchi kuwa usalama upo wa kutosha na siku ya kesho wataimarisha usalama zaidi 

Amesema kanisa hilo la TAG wanalipenda kwasababu Askofu wake mkuu ni mtu mzuri,hana makuu,na ni mtu ambaye viongozi wa serikali wanamuheshimu,hivyo ni mfano mzuri wa kuigwa hata na viongozi wengine wa kidini.

Amesema kuwa wale ambao wakisikia neno la Mungu linahubiriwa wanasema ni kelele mapepo washindwe, kwani Mtu yeyote akikwambia huwezi kufanikiwa wewe jitikise kama punda utajitikisa mwisho utajikuta upo juu.

Kwa upande wake muhubiri huyo kutoka nchini Sweeden Johannes Amrizer amemshukuru mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwa kumtia moyo akiwa katika mkoa huo wa Arusha

Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: