Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akikagua moja ya vyumba vya mahabara katika shule hiyo mpya inayotazamiwa iliyopo katika kata ya Olasiti mkoani hapa kuingiza wanafunzi kuanzia januari mwakani 2020.Picha/Habari na Vero Ignatus
Mkuu wa mkoa Mrisho Gambo akielekea kukagua msingi wa ujenzi wa nyumba xa Waalmu katika shule mpya ya sekondari ya Mrisho Gambo ambayo inatazamiwa kuanza kuingiza wanafunzi januari mwakani 2020.

 Msingi wa nyumba za Waalimu katika Shule mpya ya Sekondari ya Mrisho Gambo kama ubavyoonekana katika picha.
 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akipokea mabati yenye thaman ya takribani milioni.15 mkurugenzi mtendaji wa kutoka  Kampuni ya Mount Kilimanjaro Safari Club George Ole Meing'arrai .
 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akimkabidhi Afisa Tarafa Mabati mara baada ya kuyapokea kutoka  ya Mount Kilimanjaro Safari Club.
 Diwani wa Kata ya Olasiti Alex Marti akizungumza na cwasndishi.wa habari katiks eneo la shule mpya ya Sekondari ya Mrisho Gambo.
Afisa Tarafa ya Elerai  Titho Maulilyo Cholobi  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa mabati ya kuezekea shule ya sekondari ya Mrisho
 Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Mount Kilimanjaro Safari Club George Ole Neing'arrai akizungumza na waandishi ww habari mara baada ya kukabidhi mabati yenye thamani ya takribani Mil.15 katika shule ya Sekondari ya Mrisho Gambo.
Mkuu wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua madarasa pamoja na ujenzi unaoendelea katika shule mpya ya Sekondari ya Mrisho Gambo iliyopo katika kata ya Olasiti mkoani hapo.

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amepokea mabati yenye thamani ya takribani milioni 15 kutoka kwa  Kampuni ya Mount Meru Kilimanjaro Safari Club ya Jijini Arusha.

Akizungumza baada ya kupokea mabati hayo amesema mwaka jana 2018 Jiji la Arusha lilipata changamoto kubwa ya wanafunzi zaidi ya  10,000 kukosa  madarasa ya kusoma katika hivyo mkoa ukadhamiria kushirikiana na wilaya zote kujenga shule ya hiyo ambayo itakayoweza kuwachukua wanafunzi watakaokaa sawasawa na matakwa ya serikali 

Amesema kuwa hadi sasa wanajenga madarasa 8 yenye maabara 3 za sayansi ,kemia,bayolojia na Fizikia lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto kwa waalimu wa sayansi katika nchi ya Tanzania.

Mhe.Gambo amesema kuwa changamoto ya walimu wa sayansi ni kubwa hivyo wameona wanapojenga shule lazima watengeneze miundombinu kwa wanafunzi kusoma masomo ya sayansi kwa vitendo.

Victoria Moshi ni Afisa ustawi wa jamii Kata ya Olasiti amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo utasaidia sana katika kipengele cha ulinzi wa ntoto kwani hawataenda mbali kufuata elimu na wazazi pia watanufaika kwani hawatakuwa na hofu juu ya usalama wawatoto wao.

Wameahidi kwamba wataendelea kuihamasisha jamii ili waendelee kushiriki katika kuchangia maendeleo ya shule katika nyanja mbalimbali na katika kuitunza shule hiyo ili kizazi kijacho nao wanufaike kwa kupitia shule hiyo. 

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji kutoka Kampuni ya Mount Kilimanjaro Safari Club amesema amemshukuru mkuu wa mkoa kwa.kuwashirikisha kama wakala wa utalii katika maendeleo ya jamii ikiwepo maswala ya Elimu .

Amesema kuwa wataendelea kuwepo kushiriki ambapo ametoa wito kwa sekta mbalilimbali iki nyingine za kiraia kushiriki ikiwemo ya Madini utalii na sekta mbalimbali wajitokeze kushiriki katika swala la maendeleo haswa sekta ya elimu. 

Amesema kuwa azma ya nchini ua Tanzania watoto wapate maeneo ya.kusoma na wapate elimu bora kwa kuboresha madarasa,mahabara na mazingira ya kumvutia mtoto.

Mwisho.
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: