Wednesday, 24 July 2019

PROFESA J KULIWASHA MOTO JUKWAA LA MISS ZONE _ARUSHA.


Na Lucas Myovela_ARUSHA

Mbunge wa jimbo la Mikumi Joseph Haule (Prof Jay ) anatarajiwa kutumbuiza katika shindano la kumsaka mlibwende wa kanda ya Kaskazini linalotarajiwa kufanyika July 27 Katika  ukumbi wa Naura Spring Jijini Arusha

Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini hapa mkurugenzi wa kampuni ya kismat promotion media Ltd , ambaye pia ni Mkurugenzi wa mashindano haya Mary Mollel Alisema kuwa jumla ya warembo 12 waliotoka katika mikoa ya kanda ya Kaskazini ambayo ni Arusha, Tanga, Kilimanjaro na Manyara wanatarajiwa kuchuana vikali ili kumpata mshindi mmoja wa miss kaskazini ambaye ambaye atawakilisha katika kinyang'anyilo cha kumpata misss Tanzania.

Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa mbali na Profesa Jay  kutoa burudani, Pia kutakuwa na wasanii mbalimbali kutoka Kanda ya Kaskazini zikiwemo ,burudani kutoka katika vikundi vya ngoma Za asili pamoja na wasanii chipkizi wenye vipaji vya kukata na shuka kutoka jiji la Arusha.

Ikiongea na warembo hao afisa Utamaduni jiji la Arusha Benson Maneno aliwahamasisha warembo hao kujiandikisha Katika daftari la kudumu la kupiga kura kwani kwa kutokufanya hivyo watapoteza haki yao ya msingi ya kupiga Kura na kutokuwa wazalendo kwa taifa lao.

"pia napenda kuwasihi muwe na hekima na heshima na nidhamu pia pindi mnapokuwa katika kambi zenu, muheshimu Jamii inayowazunguka pamoja na viongozi wanaowafundisha ,napia napenda kuwaasa muwe natabia Mjema maana nyie nimfano wa kuigwa katika Jamii naweza sema nikioo cha jamii na jamii nzima inawaanhalia nyie pia wadogo zenu wanao tamani kushiriki katika mashindano hayo "Alisema Benson Maneno

Kwa upande wake mrembo wa kanda ya Kaskazini anaeachia muda wake Teddy Mkenda Alisema mashindano haya yamemsaidia mambo mengi ikiwemo kuvijua vituo mbalimbali vya utalii vilivyopo hapa nchini.

Hata hivyo aliwataka warembo hao kujiamini na kutumia taaluma yao na urembo huo kusaidia Jamii inayowazunguka, huku akiwataka kujitaidi ili waweze kuleta taji la miss Tanzania ndani kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment