Serikali ya wanafunzi ya Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere imesisitizwa  kutambua Sheria, kanuni na taratibu wakati wote inapotekeleza majukumu yake ya uongozi, ikiwa ni pamoja na wanafunzi kuacha njia za mkato za kughushi, kubadilishana vitambulisho pamoja na kujiepusha na makundi ya uchachochezi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Chuo hicho Prof. Shadrack Mwakalila wakati alipokuwa akifungua
mafunzo maalumu yakujewangea uwezo viongozi wapya wa serikali ya Wanafunzi katika uendeshaji wa Serikali ya Wanafunzi pamoja na Chuo kwa ujumla.

Prof. Mwakalila amesema Serikali ya Wanafunzi ni chombo muhimu katika uendeshaji wa Chuo kwani ni kiwakilishi na daraja muhimu baina ya wanafunzi na uongozi wa chuo, hivyo  ni muhimu kuwa na mafunzo ya  kujengeana uwezo katika utekelezaji wa majukumu hayo muhimu.

“Ninatambua wazi kuwa Serikali ya Wanafunzi inafanya kaz ikwa mwaka mmoja na ina Wizara mbalimbali zinazo akisi mahaitaji na huduma ambazo wanafunzi wanahitaji wakiwa katika masomo yao hapa chuoni, hivyo ni muhimu kwa viongozi hao kutambua wajibu wao  Serikali yao na kwa wanafunzi wenzao  chuo,”alisisitiza Prof. Mwakalila.

 Prof. Mwakalila amesema  kuwa, ili kuwa kiongozi katika Serikali ya Wananfunzi ni lazima mwanafunzi awe awe ametimiza vigezo vyote ikiwa ni pamoja na kulipa ada, kufaulu mitihani , nidhamu na uaminifu, kwa  misingi hiyo basi, kuwa Kiongozi haiondoi majukumu, wajibu na matakwa ya kuwa mwanafunzi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

“Tunaelewa kuwa kiongozi anatakiwa kuongoza kwa mujibu wa sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa, Kwenye kiapo chenu cha utii mliahidi kulindana kutunza siri za serikali na chuo, kufuata na kutii sheria na taratibu za Chuo na Nchi, hivyo ni jukumu lenu kutimiza hayo yote kwa weledi,” alisema Prof. Shadrack Mwakalila.

Mafunzo ambayo wanapatiwa viongozi hao wa serikali ya wanafunzi yanalenga kuwajengea uwezo katika utendaji kazi ikiwa ni pamoja na uongozi wenye uwajibikaji, maadili ya uongozi, utatuzi wa migogoro, taratibu za fedha za umma na matumizisahihi, mawasiliano na matumizi ya muda.

Aliwataka pia viongozi hao wa wanafunzi kuwahimiza wanafunzi wenzao kulipa ada na michango mingine kwa wakati, wanafunzi waache njia za mkato za kugushi na kuazimana vitambulisho, kwani Kugushi ni kosa la jinai hivyo kila atakaye  tenda kosa hilo sheria itachukua mkondo wake.

Prof. Mwakalila amekemea kuwepo kwa vitendo vya  udanganyifu katika mitihani huku akiwataka  wanafunzi Kukumbushana kusoma kwa bidii kwani ndiyo jambo la msingi lililowapeleka chuoni hapo, huku akiwakumbusha twanafunzi kuwa waadilifu na wazalendo na kujiepusha na tabia yoyote inayoweza kuhatarisha utulivu na Amani  chuoni hapo.

Prof. Mwakalila pia amewataka viongozi wa serikali ya wanafunzi  kuchuja na kuhakiki taarifa zote kabla yakuzipeleka kwa umma  ambapo amesisitiza kuwa Kiongozi makini ni yule ambaye anafuatilia jambo na kujiridhisha kabla ya kuchukua hatua ilikuepusha uvunjifu wa amani kwa mambo yasiyo ya lazima.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: