Friday, 5 July 2019

NMB WAKABIDHI MSAADA CHUO CHA MWALIMU NYERERE


Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere- MNMA leo kimepokea msaada wa Projector 1 na Podium 1 ambazo zitatumika katika ufundishaji na kuleta ufanisi katika sekta ya elimu.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo kutoka benki ya NMB Naibu Mkuu wa Chuo taaluma, utafiti na ushauri wa kitaalamu Prof. Richard Kangalawe amesema vifaa hivyo vitawasaidia wahadhiri kutumia Teknolojia ya kisasa na hivyo kurahisisha ufundishaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi za kibenki - NMB William Makoresho amesema lengo la msaada huo ni kuongeza chachu katika kuboresha utoaji wa mafunzo na kuongeza ufanisi.

Makoresho amesema katika kusogeza Huduma zao karibu na wananchi NMB imefika msaada huo ambao unakwenda sambamba na kauli mbiu ya benki hiyo unaosema “ Daima karibu yako” na hivyo kudhihirisha kuwa NMB ipo karibu na Chuo Cha Mwalimu Nyerere.

Imetolewa na:

Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
5/7/2019

No comments:

Post a Comment