NAIBU Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Msafiri Mbibo akizungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo kituo cha Forodha Horohoro wilayani Mkinga mkoani Tanga mpakani mwa Tanzania na Kenya wakati wa ziara yake kushoto ni Kamishna Msaidizi Ushuru wa Forodha na Bidhaa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Benard Asubisye kulia ni Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure
 Kamishna Msaidizi Ushuru wa Forodha na Bidhaa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Benard Asubisye akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo
 Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza wakati wa ziara hiyo
 Afisa Mfawidhi wa Kituo cha forodha Horohoro Bakari Athuman akizungumza wakati wa ziara hiyo
 NAIBU Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo kulia akionyeshwa kitu na Afisa Mfawidhi wa Kituo cha forodha Horohoro Bakari Athuman wakati wa ziara yake
  NAIBU Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo  katikati akiingia mpakani mwa Tanga na Kenya eneo la Horohoro wakati wa ziara yake kulia ni Afisa Mfawidhi wa Kituo cha forodha Horohoro Bakari Athuman wakati wa ziara yake
NAIBU Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo kushoto akisalimiana na  Afisa Mfawidhi wa Kituo cha forodha Horohoro Bakari Athuman mara baada ya kufika eneo la Horohoro wilayani Mkinga  mpakani mwa Tanzania na Kenya wakati wa ziara yake kulia ni Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure
 Sehemu ya watumishi wa mamlaka hiyo wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo
 Sehemu ya watumishi wa mamlaka hiyo wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo
 Sehemu ya watumishi wa mamlaka hiyo wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo

NAIBU Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Msafiri Mbibo amesema kwamba wanatarajia kukifanya kituo cha Horohoro kuwa kituo cha pamoja (One Stop Board Post) ili kiweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

Mbibo aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea kwenye kituo hicho cha forodha kilichopo mpakani kwa Tanzania na Kenya eneo la Horohoro wilayani Mkinga mkoani Tanga ikiwemo kuzungumza na watumishi sambamba na kukikagua kituo hicho.

Alisema yapo mambo machache wanayokamilisha kabla ya kituo hicho kuanza kazi hivyo kuhaidia kwenda kuyashughulikia  kwa haraka kwa kuwasiliana na taasisi, mamlaka nyengine ikiwemo upande mwengine wa wenzao wa nchi jirani ya Kenya ili kuhakikisha kwamba kituo hicho kinafanya kazi kama ilivyokusudiwa.

“Lakini pia nimeambiwa changamoto ya Jenereta nimeambiwa inafanyiwa kazi na inakaribia kukamilika tutakaporudi dar tutahakikisha vifaa hivyo vinafika na kufungwa suala la uhakika wa umeme litakuwa sio tatizo tena na suala la maji litashughulikiwa”Alisema

Hata hivyo aliwataka watumishi wa umma kwenye kituo hicho kuhakikisha wanashirikiana kwenye kufanya kazi na kutanguliza uzalendo kwenye shughuli zao ili kufikia malengo ambayo yamekudiwa.

Naibu Kamisha huyo alisema kwamba nchi haiwezi kuendelezwa na mtu mwengine isipokuwa watanzania wenyewe na kila mtanzania sehemu aliyopo afanye kazi kwa kiwango cha juu ili waweze kuyafikia malengo yao.

Hata hivyo pia aliwataka watumishi wa mamlaka hiyo kwa nchi nzima kuhakikisha wanakuwa waadilifu kwa kiwango cha juu kwa sababu ndio silaha ya mafanikio yoyote na kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Kamishna Msaidizi Ushuru wa Forodha na Bidhaa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Benard Asubisye alionyeshwa kushangazwa na ukusanyaji wa mapato kwenye kituo cha Forodha cha Horohoro wilayani Mkinga kushuka kutoka bilioni 25 hadi 23.

Hiyo ilitokana na taarifa iliyotolewa na Afisa Mfawidhi wa Kituo cha forodha Horohoro Bakari Athumani kuonyesha kushuka kwa kiwango cha ukusanyaji wa mapato

Katika taarifa yake Afisa Mfawidhi huyo alimueleza Naibu Kamishna huyo kwamba alisema mwaka wa fedha 2017/2018 walifanikiwa kukusanya kiasi cha Bilioni 25 lakini mwaka wa fedha 2018/2019 ukusanyaji huo ulishuka mpaka kufikia bilioni 23 jambo ambalo liliwashutua viongozi hao.

Alisema kwamba waliosoma masomo ya sayansi hiyo sio kupanda badala yake wana shuka chini na sio kwenda mbele bora wangebaki kwenye makusanyo ya awali ili waangalie namna ya kujipanga kuongeza mapato.

Mwisho.
Share To:

Post A Comment: