Na Lucas Myovela_Arusha.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha Dr Charles Wilson Mahera,ameeleza katika halmashauri yake changamoto ya maji inakwenda kupungua kama siyo kumalizika kabisa katika halmashauri ya Arusha endapo mradi mkubwa wa maji wa bilioni 520 unaotekekezwa na jiji la Arusha kupitia idara ya maji ya mkoa AUWASA.

Dr mahera ameeleza hayo wakati akiongea na wazee wa halmashauri hiyo katika kongamano maalum la wazee lililo andaliwa kwa lengo la wazee kuwasilisha kero zao na changamoto zinazo wakabili na kuishauri serikali pamoja na viongozi wa halmashauri hiyo katika utendaji kazi.

Mahera ameeleza kwamba licha ya wilaya ya arumeru kuwa na maji ya kutosha kwa baadhi ya maeneo lakini mradi huo wenye uwezo wa kutoa lita milioni 200 kwa siku na huku matumizi ya jiji la Arusha ni lita milioni 94 na maji yanayo baki yataelekezwa katika wilaya ya Arumeru na kuzifikia kata 21 zenye wakazi 143,770 huku pia katika wilaya Hai Mkoani kilimanjaro na Simanjiro Mkoani Manyara kufaidika na mradi huo.

"Katika mradi huu mkubwa wa maji tunategemea utaweza kutatua kero kubwa ya maji ambayo ni kwa baadhi ya maeneo yetu hapa Arumeru kwa kuzifikia kata za  Kimnyaki,Makiba,Mbuguni,Kikwe,Chekereni,Olimotonyi,Ambureni,Akeri,Selasing'isi,Poli,Nkoaranga,Nkoanekori,Imbasenyi,Kiranyi,Kiutu,Moivo,Matevesi,Mbangata,Kisongo,Sokoni II pamoja na Oleirieni." alisema Dr Mahela.

"Licha ya maeneo mengi ya wilaya ya Arumeru kuzungukwa na maji na milima bado tunayo changamoto ya ubovu wa barabara na viongozi mlio wachagua bado hawajawa chachu kuwaletea maendeleo wazee wangu ila serikali ya awamu ya tano ya Dk John Pombe Magufuli inapambana sana kuhakikisha mnapata huduma bora serikali inaendela kuboresha huduma za Afya,Elimu na Miundombinu sahihi kwa wananchi wake na mimi kama mkurugenzi wa Halmashauri hii ninasimamia ipasavyo fedha ya serikali inayo kuja kwaajili ya maendeleo ifanye kile ilicho kusudiwa ili Arumeru yetu izidi kukua." aliendelea kusema Dr Mahela.

Awali wazee hao wakitoa kero zao kubwa za shida ya maji kwa baadhi ya maeneo,ubovu barabara na matibabu katika wilaya hiyo wameiomba serikali ya awamu ya tano kuwapa kipaumbele kwa kuwaundia mipango sahihi ya upatikanaji wa huduma ya afya pamoja na dawa muhimu.

"Kwanza naishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuzidi kuchapa kazi na pongezi zetu ziende kwa Dr John Magufuli sisi tupo pamoja nae na zingine kwako wewe Mkurugenzi wetu na mwisho kwa mkuu wa wilaya,Mimi nina shida moja ukienda katika kituo cha Afya kweli matibabu unapewa bure lakini kwenye upewaji wa dawa muhimu nyingi hatupewi na tunaandikiwa tukanunue nje ambapo huko zinauzwa bei kubwa sana kiasi wengi wetu hatuwezi kumudu na pia barabara zetu sio rafiki sana hata ukiugua ghafla hadi kuja kufika hospital imechukua muda." alisema mmoja wa wazee hao.

Nae kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry muro kwa kufuatilia kero hizo ametoa maelekezo kwa wahudumu wa vituo vya Afya,zahanati na hosptali kubwa za wilaya hiyo pindi wazee wafikapo kupata hiduma ni vyema kuwahudumiwa kimatibabu kwanza ndipo waanze kufuata mlolongo mwingine na kurleza kwamba kwa mwaka huu serikali tayari imetenga fedha za kutosha kwaajili ya madawa maalumu,Pia katika swala la miundombinu amelipokea na kuhaidi kulifanyia kazi.

"Niwaombe wazee wangu serikali inawapa matibatu bure na swala hili la miundombinu ni haki ya kimsingi ila viongozi mlio tuchagulia sio wa maendeleo na wala siyo wa kasi ya awamu hii madiwani wengi mmewapa kura nyie na ndiyo wanawaangusha wala siyo serikali niwatake tu kwa kipindi kijacho msisitee kuchagua viongozi maana mitambo tunayo ila madiwani wenu wanapokaa katika baraza wanaamua kuikodisha mitambo hiyo wilaya zingine na kuziacha kata zao zikiwa chakavu wao hujali maslahi yao binafsi na siyo yenu nyinyi wapiga kura." alisema Dc Muro
Share To:

msumbanews

Post A Comment: