Mbunge
wa Jimbo la Singida Magharibi, Eribariki Kingu, akizungumza na Wajumbe
wa nyumba kumi (mabalozi) wa Kata ya Mkalawa katika mkutano wa ndani
wilayani Ikungi mkoani Singida jana.
Mbunge
wa Jimbo la Singida Magharibi, Eribariki Kingu (mwenye miwani walio
simama), akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa nyumba kumi
(mabalozi) wa Kata ya Mkalawa baada ya kufanya nao mkutano wa ndani
wilayani Ikungi mkoani Singida jana.
Mbunge
wa Jimbo la Singida Magharibi, Eribariki Kingu akizungumza na Wataalam
wanao simamia mradi wa maji wa Tanjet uliopo Kata ya Mkalawa. Mradi huo
umeletwa kwa jitihada za Mbunge huyo.
Mbunge
wa Jimbo la Singida Magharibi, Eribariki Kingu (mwenye miwani ), akiwa
katika picha ya pamoja na Wananchi wa Kijiji cha Nkurusi baada ya
kufanya nao mkutano wa hadhaa wilayani Ikungi mkoani Singida jana.
Mbunge
wa Jimbo la Singida Magharibi, Eribariki Kingu, akiwa na Walimu wawili
pekee wa kujitolea wa Shule ya Msingi ya Ishingisha aliowaahidi kuwapa
sh.milioni 1.5 kutoka katika mfuko wa jimbo kama motisha. Kushoto ni
Mwalimu Daniel Michael na Mwalimu Augustinho Kitiku.
Mbunge
wa Jimbo la Singida Magharibi, Eribariki Kingu (mwenye miwani ), akiwa
katika picha ya pamoja na Wananchi na Wanafunzi wa Kijiji cha
Ishingisha baada ya kufanya nao mkutano wa hadhara wilayani Ikungi
mkoani Singida jana.
WANANCHI
wa Kata ya Makilawa wilayani Ikungi mkoani Singida wamesema wameanza
kusafisha magodoro yao baada ya kupata maji kupitia mradi wa Tanjet.
Hayo
yalibainishwa juzi na Katibu Mwenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Kata ya Makilawa Stuu Babu wakati akizungumza mbele ya Mbunge wao
Eribariki Kingu alipofanya ziara ya kutembelea kata hiyo na kuzungumza
na wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo pamoja na
kuwahamasisha kujitokeza kwa wingi kujiandika katika daftari la kudumu
la mpiga kura na kuhakikisha CCM inapata ushindi kwenye chaguzi zake.
"Kwa
kweli tunampongeza mbunge wetu kwa kazi kubwa anayoifanya katika jimbo
letu kwani tangu kijiji chetu kianzishwe mwaka 2002 hatukuwahi kuwa na
maji lakini amefanikisha kutuletea maji kupitia mradi wa Tanjet ambapo
tumeweza kusafisha na magodoro yetu" alisema Babu.
Diwani
wa Kata hiyo Shabani Hassan alisema katika kutekeleza ilani ya CCM,
Mbunge huyo ameweza kuchangia zaidi ya sh.milioni 20 katika shughuli
mbalimbali za maendeleo jambo ambalo halikuwa kufanywa na wabunge watangulizi wake.Katika
ziara hiyo aliyoifanya na kutembelea baadhi ya vitongoji katika Kata za
Makilawa na Iglanson aliweza kukagua miradi ya ujenzi wa shule na
kuahidi fedha za kukamilisha miradi hiyo.
Katika
hatua nyingine Kingu aliahidi kutoa sh.milioni 1.5 kutoka katika mfuko
wa jimbo kama motisha kwa walimu wawili pekee wa kujitolea wa Shule ya
Msingi ya Ishingisha kwa moyo wa uzalendo wa kujitolea kufundisha shule
hiyo tangu ikiwa haina wanafunzi na sasa inawanafunzi 192.
Post A Comment: