Friday, 26 July 2019

Mbunge Bonah ameitaka Serikali kutenga fungu kwa ajili ya Majukwaa ya wanawakeNA HERI SHAABAN

MBUNGE wa Segerea (CCM)Bonah Ladslaus  ameitaka Serikali kuyatengea fungu maalum Majukwaa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yaliopo Wilaya ya Ilala.


Bonah aliyasema hayo Katika uzinduzi wa Jukwaa la 13 la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Kata ya Kimanga Manispaa ya Ilala leo.

"Nimefarijika  kushiriki kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Jukwaa la Kimanga na kuangalia fursa mbalimbali za Wanawake changamoto kubwa nimeona majukwaa hayana fungu
 kwa ajili ya kujiendesha naomba serikali  waweke fungu lao kwa ajili ya kujiendesha "alisema Bonah.


Bonah alisema katika wilaya ya Ilala Wanawake wengi wana muamko wameweza kuzindua majukwaa ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi lakini wanashindwa kusonga mbele kutafuta fursa kutokana na majukwaa yenyewe bado kutengewa fungu maalum.

Alisema atalibeba kama Mbunge wa Segerea kwenda kulizungumzia katika vikao kwa nafasi yake ya Mbunge ili waweze kuyatambua katika bajeti ili yaweze kujiendesha .

Aidha alisema Jukwaa ni sehemu ya fursa mbalimbali za biashara ,amewataka Wanawake kuchangamkia fursa na kutafuta masoko ya biashara ili waweze kujikwamua kiuchumi.


Aliwataka Wanawake wa Wilaya ya Ilala wa Jukwaa kushirikiana ili wajikwamue Kiuchumi waache maisha tegemezi.

Alimpongeza Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli  ya Tanzania ya Viwanda kwa  Utekelezaji wa Ilani  kuwawekea misingi mizuri Wanawake katika fursa mbalimbali.

Pia Bonah alielezea baadhi ya vikundi vilivyochukua mikopo Jimbo la Segerea  alisema Vingunguti vikundi 58, Kipawa 60, na Segerea 48.ameviagiza vikundi vingine vilivyopo Jimboni humo kuchangamkia fursa ya Mikopo ya Serikali ya asilimia kumi ya Wanawake,Vijana na Watu wenye Ulemavu.

Kwa upande wake Katibu wa Jukwaa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Kata ya Kimanga Joyce Exaud  alisema Jukwaa la Kimanga ni kiunganishi muhimu kwa wanawake wote wa kata hiyo ili kuakikisha wanazitumia vyema fursa za ujasiriamali katika kuakikisha wanajifunza kwa ubora na kupeana fursa kwa kufanya biashara zenye tija kwa kuongeza thamani ya biashara zao.

Katibu Joyce alisema pia jukwa hilo litawasaidia kujifunza njia bora zs kutafuta kupanua masoko ya biashara zao.

"Kata ya kimanga ina vikundi vilivyossjiliwa 96 vilivyoomba mikopo halmashauri vipo 34  vilivyopata mikopo 11vikundi vyote vya wanawake "alisema Joyce.Naye Diwani wa kata ya Kimanga Manase Mjema, alitoa fursa kwa Wanawake wa Jukwa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Kimanga, Aliagiza kuandika barua kwa ajili ya kuomba tenda ya usafi amewataka wafuate taratibu ofisi ya Kata kupitia kwa Ofisa Maendeleo ili waweze kupata tenda za usafi.

MWISHO

Tabata Kimanga Julai 25/2019

No comments:

Post a Comment