Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe(Katikati) akizungumza katika kikao cha Mawaziri wa Serikali ya Tanzania bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wanaosimamia Sekta za Utalii, Habari, Utamaduni, Sanaa, Michezo na Mambo ya Kale kilichofanyika Julai 02, 2019 Jijini Dodoma. Kushoto ni Balozi Ally Abeid Karume na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale na kulia ni Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo.
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Vijana,Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ally Abeid Karume na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo (Kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar) wakisaini Taarifa ya Ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika Sekta wanazosimamia leo Julai 02,2019 Jijini Dodoma.Wanaoshuhudia ni Viongozi waandamizi wa wa Jamhuri ya Muungano katika Sekta hizo.
 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya  Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nicholas William akizungumza katika kikao cha Mawaziri wa Serikali ya Tanzania bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wanaosimamia Sekta za Habari, Utalii Utamaduni, Sanaa, Michezo na Mambo ya Kale kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika sekta hizo kilichofanyika Julai 02,2019 Jijini Dodoma.
 
Baadhi ya Washiriki  wa kikao  cha Mawaziri wa Serikali ya Tanzania bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wanaosimamia Sekta za Habari, Utalii Utamaduni, Sanaa, Michezo na Mambo ya Kale kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika sekta hizo wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika Julai 02,2019 Jijini Dodoma.
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Wanafunzi na wanamichezo  wa shule ya Foutain Gate Academy iliyopo Jijini Dodoma ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kukuza vipaji mbalimbali vya michezo wakati akiwatambulisha Waziri wa Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo Balozi Ally Abeid Karume (kulia)  na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo (wa pili kulia) kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar walipoitembelea shule hiyo leo Julai 02, 2019.
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt Harrison Mwakyembe (kushoto) akiwatambulisha Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ally, Abeid Karume (kulia)  na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo (wa pili kulia) kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa Wanafunzi na wanamichezo wa shule ya Foutain Gate Academy iliyopo Jijini Dodoma ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kukuza vipaji mbalimbali vya michezo walipoitembelea shule hiyo leo Julai 02,2019.
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ally Abeid Karume, Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na viongozi waandamizi wanaosimamia Sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Uongozi na Wanafunzi na wanamichezo wa shule ya Foutain Gate Academy iliyopo Jijini Dodoma ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kukuza vipaji mbalimbali vya michezo walipoitembelea shule hiyo leo Julai 02, 2019.
 
Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akifurahia zawadi ya sabuni aliyopewa na Uongozi wa wa Shule ya Foutain Gate Academy mara baada ya kuitembelea shule hiyo iliyopo Jijini  Dodoma leo Julai 02, 2019.  (PICHA NA SHAMIMU NYAKI- WHUSM).
Share To:

msumbanews

Post A Comment: