Thursday, 11 July 2019

MAABARA YA KUTEMBEA YA KUFANYA UTAFITI WA KUPIMA UBORA WA UDONGO KABLA YA KULIMA YAZINDULIWA RASMI ARUSHA

 Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega watatu kulia , Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi Marjolyn kutoka nchini Uholanziwa tatu kushoto  ,pamoja na  Dkt Edmond Matafu wa kwanza kulia pamoja na viongozi wengine  wakikata utepe ikiwa ni ishara ya maabara hiyo ya kutembea imezinduliwa rasmi.
  Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega pamoja na  Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi Marjolyn kutoka nchini Uholanzi wakikata utepe ishara ya kufungua rasmi maabara za utupimaji wa udongo

  Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akipeana mkono na  Dkt Edmond Matafu ambaye ni moja wa wawekezaji walioleta maabara hiyo ambayo itaidia sana wakulima kwani watakuwa wanapima udongo huo kabla ya kulima .
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akiongea jambo mara baada ya kuzindua maabara hiyo ya upimaji wa udongo.
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amezindua Maabara ya kutembea ya kufanya utafiti wa kupima ubora wa udongo kwa wakulima ili kupata uhakika wa kuwa na mazao mengi yenye ubora kwa kutumia teknolojia hiyo mpya ya upimaji wa Udongo iliyoletwa kutoka nchini Uholanzi na Mtanzania Dkt.Edmund Matafu Makazi wa jijini Arusha.

Amesema kuwa Teknolojia hiyo ambayo ni yakwanza hapa nchini, itakuwa mkombozi kwa mkulima na kuongeza mapato na uzalishaji kwa kujua jiografia,eneo na udongo,kwani thamani ya malipo ya upimaji huo ni rafiki kwa wakulima kuchangamkia fursa ya upimaji.
 Kwa upande wake ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya   live  support systerms limited inayojishuhulisha na shuhuli ya upimaji wa  udongo pmoja na utengenezaji wa Mbolea  Tanzania Dkt Edmond Matafu alisema maabara hiyo itawasaidia kubaini virutubisho na muundo wa udongo wa eneo husika ,hivyo kumwezesha mkulima kujua mazao gani yanayostahili kulimwa katika eneo husika na kuepuka kilimo cha kubahatisha ambacho kimekuwa kikiwaletea hasara wakulima walio wengi nchini.
‘’Maabara hii tulianza kuitumia nchini Kenya na sasa imeingia nchini na imekuwa na manufaa makubwa kwa wakulima kuweza kubaini mapungufu katika udongo na jinsi ya mahitaji ya mbolea’’.Alisema dkt Matafu
Alibainisha kuwa kabla ya kuzindua maabara hii watanzania walikuwa wanakosa huduma hii  kwa hapa nchini kwani walikuwa wanalazimika kwenda hadi nje ya nchi ikiwemo Kenya kupima udongo huo

Alisema kuwa huduma hii itamnufaisha mkulima kutokana na kupata mazao mengi mara baada ya kupima udongo ambao anataka kulima na baadae kupewa ushauri ni mbolea gani itakayomsaidia kumpa mavuno mengi,na pia itamsaidia kupunguza upotevu wa fedha kwani atakuwa analima sehemu ambayo kaipima pia atakuwa amepewa anunue mbolea gani itakayo msaidia.

No comments:

Post a comment