NA HERI SHAABAN
MKURUGENZI wa Kampuni ya Udalali Yono Action Mart Scholastika Kevela amewataka Wanawake wa Wilaya ya Ilala kujitambua ili waweze kuwa wajasiriamali wazuri.
Kevela aliyasema hayo kata ya Tabata Manispaa ya Ilala wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi .
" Nawapongeza Wanawake wa Tabata kwa uzinduzi wa Jukwaa lenu naomba Wanawake wa Wilaya ya Ilala wote kujitambua ili muweze kujikwamua kiuchumi muachane na maisha tegemezi "alisema Kevela.
Kevela aliwataka Wanawake kuwamka kwani Mwanamke ndio Waziri Mkuu anaongoza nyumba anayo mamlaka yote ndani ya familia .
Alitumia nafasi hiyo Kumpongeza Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli ya Tanzania ya Viwanda ambayo imesaidia kwa asilimia 100 kusaidia vikundi mbalimbali kuviwezesha mikopo ya asilimia 10 ambayo inatolewa ngazi ya halmashauri.
Alisema Jukwaa ni sehemu ya fursa halina ubaguzi ,aliwataka Wanawake kushikama na kuwa wamoja rafiki wa Mwanamke ni mwanamke mwenzake.
Kwa upande wake Mratibu wa Dawati la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Wilaya ya Ilala Georgis Asenga, alitoa elimu ya jukwaa na maana yake.
Pia Asenga alivitaka vikundi vikamilishe taratibu za usajili ili viweze kupewa mikopo ngazi ya halmashauri.
Alisema mpaka sasa katika manispaa ya Ilala jumla majukwaa 11 yamefanikiwa kuzinduliwa bado kata 25 zipo katika taratibu za uzinduzi wake.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa Wilaya ya Ilala Sauda Addey amewataka Wanawake kushirikiana kwa pamoja katika shughuli zao za kiuchumi waanzishe viwanda vidogo vidogo katika wilaya ya Ilala .
Sauda alisema imefika sasa wakati Wanawake kujishughulisha wainuke kiuchumi, wasiweke chuki katika vikundi wawe wamoja waheshimu viongozi waliochaguliwa kwa ajili ya kuwaongoza.
Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Kata ya Tabata Agines Minzi alisema Kata ya Tabata ina vikundi 294,vilivyosajiliwa 182 ,vilivyopewa mikopo 22 ,vikundi 76 vinatarajia kupata mikopo vya Wanawake 51,vijana 25 vya Walemavu 10.
Agines alisema vikundi vilivyokuwa katika mchakato vipo kumi vishatuma maombi Wanawake 30 vijana 20 walemavu watano.
MWISHO
Post A Comment: