Na Heri Shaaban
MKOA wa Dar es Salaam leo umekabidhi vikombe vya Ubingwa wa Mashindano ya Umoja wa Shule za Sekondari (UMISSETA )ngazi ya Taifa mara baada kuibuka mabingwa katika mashindano hayo yalioisha hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Ofisa Elimu Sekondari mkoa huo Hamiss Lissu alisema  katika mashindano ya UMISSETA ngazi ya Taifa mwaka huu  ambapo Dar es Salaam wamechukua ushindi huo kwa mara ya tatu.

"Mkoa wangu wa Dar es Salaam umefanya vizuri katika mashindano haya toka mwaka 2017 tupo vizuri sekta ya michezo  tunashika namba moja " alisema Lissu.

Aidha Lissu alisema katika mashindano ya Umoja wa shule za Msingi UMITASHUMTA mkoa huo wake umeshika nafasi ya pili Taifa kufuatia nafasi ya kwanza kuchukuliwa na Mkoa wa Tabora.

Alisema katika mashindano hayo watajipanga mwakani washike nafasi hiyo ya kwanza ambayo wameipoteza mwaka huu 2019 kwa point 2 katika kipengele cha usafi ikawafanya Tabora kuibuka kidedea .

Aliwapongeza Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda,Katibu Tawala Mkoa,Walimu Wanafunzi ,Maofisa Elimu wote kwa jitihada nzuri kuakikisha tunaendelea kufanya vizuri katika mashindano ya Taifa.

Pia aliwapongeza walimu waliojitolea kwenda kuhamashisha mashindano hayo ambayo yanaanda vipaji vya watoto ili waweze kuwa wachezaji wazuri.

Alitoa wito kuandaa wanafunzi wa mkoa huo kwa ajili  ya mashindano yajayo ngazi ya mkoa hadi Taifa.

Alisema kwa sasa Wanafunzi wanaendelea na michezo mbalimbali viwanja vya Jakaya Kikwete ,Karume uwanja wa Shirikisho la Mpira Miguu TFF na  Ukonga.

Lissu alisema katika mafanikio changamoto hazikosekani ,changamoto zilizoikumba  michezo hiyo ni wanja vya michezo kutokana na shule nyingi kukosa viwanja hivyo,amezungumza na Wakurugenzi wa halmashauri zote tano kutatua changamoto hiyo katika mashindano yajayo.

Akielezea mafanikio mengine waliopata katika mashindano hayo ,wamefanikiwa vijana watano wa riadhaa wamechukuliwa  kwa ajili ya kushiriki michezo mikubwa .

Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: