Tuesday, 25 June 2019

WATOTO WILAYANI PANGANI WAZITAKA MAMLAKA ZA KISHERIA KUWACHUKULIA HATUA KALI ZA WANAOJIHUSISHA NA VITENDO VYA UBAKAJI NA ULAWITI

RAISA SAIDI ,PANGANI.

WATOTO wilayani Pangani Mkoani Tanga wamezitaka mamlaka husika za kisheria kuhakikisha zinawachukulia hatua kali za kisheria watu wanaojihusisha na vitendo vya ubakaji, ulawiti na wanaowapa mimba wanafunzi kwani wanakatisa ndoto zao na kuharibu maisha yao

Huku wakieleza kwamba watafurahi siku moja ikitokea wabakaji au wanaowalawiti wakifungwa vifungo mbalimbali kwani hivi sasa kesi ni nyingi lakini matokeo ya kesi ni madogo sana.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Funguni  Mwanaidi Ally ambapo alisema  alisema siku hizi kumekuwa na tabia ya watoto katika jamii kubakwa na kulawitiwa na watu wazima ikiwemo wengine kuwaozesha tabia ni kiyume cha sheria ya nchi.

Alisema tabia hiyo zimekuwa kikwazo kikubwa cha watoto hao na wengi kushindwa kuhitimu masomo yao na kupata mimba za utotoni na kupelekea wimbi la utegemezi kwenye familia na Taifa kwa ujumla ikiwemo kuongezeka magonjwa ya zinaa na kusababnisha kupungua nguvu kubwa ya Taifa.

“Sisi kama watoto tuna ndoto nyingi na serikali ndio kimbilio letu baada ya wazazi na walezi na jamii kukatisha ndoto zetu ,jamii itambue kumekuwa na wimbi kubwa la kubakwa na kulawitiwa watoto wa kiume wao na watu wazima hivyo tunaimba jamii ikishiriki kikamilifu kutulinda kututunza na kutuelendeleza kufikia malengo”Alisema

Katibu Tawala wa wilaya Mwalimu Hassani Nyange alisema kwamba watoto wanaokumbana na ukatili wa kijinsia na kubakwa wilayani humo ni kuanzia darasa la kwanza ,la pili la tatu na nne na kuandelea jambo ambalo ni hatari sana kwa ustawi wa maendeleo ya watoto hao.

“Hili ni ni tatizo kubwa sana OCD hapa wilayani Pangani lakini pia inaumiza sana hivyo jamii lazima ibadilike na kuhakikisha wanawafuchua watu wanaohusika na vitendo hivyo kwenye jamii lakini pia toeni ushirikiano tuweze kumaliza matukio ya ukatili wa kijinsia kiu yangu ni kuona matokeo kesi zinaendelea mahakamani yanakwisha na wahusika kuchukuliwa hatua “Alisema

Hata hivyo aliwataka wazazi na walezi kutoa ushirikiano wa kwenda kutoa ushahidi pindi yanapotokea matukio hayo msikubali kurubuniwa kwani kufanya hivyo tunapelekea haki kushindwa kutendeka na wahusika kuchukuliwa hatua

“Lakini kama mashauri mengi yatakuwa yanalalamikiwa na mashauri kushindwa kupata muafaka hiii pia sio taswira nzuri kwetu hivyo watu kwenye vyombo husika wananchi watajenga mashaka nao nao wabadilike “Alisema

Naye kwa upande wake Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi aliwataka wanaume kuwaacha watoto wa kike wasome na kupata elimu ambayo itakuwa ndio silaha kubwa kwenye maisha yao ya sasa na baadae.

Hata hivyo aliwataka watendaji wa Kata na Vijiji kuacha kumaliza kesi zinazohusiana na masuala hayo kwenye maeneo yao badala yake wahakikishe zinafikishwa mahakamani.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment