Na Lucas Myovela
ARUSHA.

Wafanya biashara wakuu katika Halmashauri ya Arusha (Arumeru),wameililia serikali kutoa elimu kwa watendaji wa chini kwa kuwakatisha tamaa wawekezaji katika upimaji wa ardhi ili kuwekeza zaidi kwa kile walichodai kujibiwa na watendaji hao kuwa Arusha haina mipango mikuu ya miji (Master Plan).

Ikumbukwe June 7/ 2019Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzajia Dk John Pombe Magufuli aliweza kukutana na wafanya biashara mbalimbali wakubwa na wakati Ikulu jijiji Dar es salaam lengo likiwa ni kuwasikiliza kero zao ili kuzitatua na kuboresha mambo mbali mbali katika uwekezaji wa ndani.

June 20 na 21/ 2019,Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Murro aliweza kukutana na wafanya hiashara wakubwa wanaofanya biashara na uwekezaji katika wilaya yake ya Arumeru huku pia lengo likiwa ni utatuzi wa changamoto wanazokutana nazo wafanya biashara katika wilaya yake na kupanga mikakati sahihi ya uwekezaji ndani ya Halmashauri hiyo ya Arumeru.

Miongoni mwa changamoto kubwa imeonekana ipo katika ardhi kitu ambacho kinafanya wawekezaji wengi kukosa nguvu ya kuwekeza zaidi ndani ya halmashauri hiyo kitu ambacho wameeleza kwamba siyo sawa kulinganaisha na pesa walizo tumia kuwekeza katika maeneo yao na kunyimwa hati za ardhi ili kupanua wigo wa uwekezaji kwa kile wanachodai watendaji wa chini wanawajibu kwamba halmashauri hiyo bado haijaingia katika master plan kitu ambacho kina kinzana na agizo la waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mh William Lukuvi.

Bw Edward N.Laiser ni mmiliki wa shule za Sinon na vyuo vya sinoni aliyewekeza katika halmashauri ya Arumeru aliye eleza mbele ya Dc Murro yeye akiwa ni muhanga miongoni mwa watu wanaozungushwa kupewa hati za umiliki wa ardhi toka mwaka 2011 alizo wekeza zenye uwekezaji wa zaidi ya Bilioni mbili kitu ambacho kinamkwamisha katika ukuzaji wa biashara yake ya elimu pindi hata anapo hitaji kuchukua mikopo mbali mbali ya kimaendeleo kukwama kutokana na kukosa hati ya umiliki wa ardhi katika sehemu alizo nunua na kuwekeza.

"Mimi ni miongoni mwa watu ninao umizwa sana na watendaji pindi ninapofuatilia swala kupimwa eneo langu nililo wekeza shule zangu pamoja na vyuo ili niweze kupanua wigo wa biashara yangu ili serikali iweze kuchukua kodi ya kutosha nakumbuka waziri Lukuvi alishatoa maelezo ma hii serikali ya awamu ya tano ni sikivu lakini watendaji wa chini wamekuwa wakinikatisha tamaa kwa kusema kwamba halmashauri hii ya Arusha haipo katika Master plani sasa nashindwa kuelewa lakini kwa vile wewe Dc wetu upo naamini hili litafikia mwisho au ukomo na kupata ufumbuzi pia swala jingine ni mrundikano wa kodi huku serikali ikiwa ni moja kodi zipo zaidi ya 12 ifikie mahali tuseme basi", Alisema muwekezaji huyo.

"Ifike hatua viongozi wetu waone Arusha inastahili kukua kwa kasi na kuongeza uwekezaji wake kwa kuondoa vikwazo kwa wawekezaji kwani inafika hatua hiashara inakuwa ngumu na kinacho tokea nikufunga biashara na nchi itakosa kodi na kushindwa kujiendesha na mwishowe uchumi wa taifa utashuka na maisha yatakuwa magumu kwa wananchi wake nimumbe Rais Magufuli azidi kuwahimiza wakuu wa wilana na wakuu wa mikoa kukutana na wawekezaji wamaeneo yao ili kutatua changamoto mbali mbali kama alivyofanaya Dc Jerry Murro", Aliendelea kusema muwekezaji huyo Edward Laiser.

Kufuatia malalamiko mengi ya wawekezaji kutokupiwa maeneo yao Mkuu wa wilaya Jerry Murro aliamua kutoa siku ya June 24 wawekezaji wote ambao tayari wanamichoro wa maeneo yao waweze kufika ofisini kwake ili kuweza kutatua tatizo hilo linaloonekana kuwa ni kinara katika ukwamishaji wa maendeleo ya wilaya hiyo huku kuwataka wataalam wa makadilio ya kodi kuwa makini katika kukadili kodi ili kuwa na unafuu kwa muwekezaji na kutoa maelekezo kwa wale wafanya wanao daiwa  wasifungiwe biashara zao na badala yake waendelee kulipa taratibu madeni yao.

Aidha pia kwa upande wa makadilio ya kodi kuwa makubwa kulinganisha na biashara husika imeonekana pia kuwa changamoto kubwa kwa wawekezaji wa Wilaya ya Arumeru hasa wawekezaji wa wa elimu (shule za binafsi) kitu ambacho wanaeleza kinawaumizwa kutokana na wazazi wengi kuwaondoa watoto wao na kuwapeleka katila shule za serikali lakini bado serikali inazidi kukadilia mapato yaleyale katika ulipaji wa kodi.

Mmilikiwa shule za St Margaret' Academy Bw Honest Tesha ameeleza kuwa uwekezaji katika elimu ni sawa na utoaji huduma za kijamii na pindi kodi zinapo kuwa kubwa ndipo wao hupandisha gharama za huduma hizo ila serikali ikipunguza gharama za kodi na gharama za huduma zitapungua kwa watanzania ili kulinganisha na huduma stahiki inayotolewa.

" Leo tumeweza kukutana hapa na mkuu wa wilaya pampoja na wakuu wa idara mbalimbali nashukuru upo hapa meneja mkuu wa TRA katika wilaya yetu ya Arumeru utaweza kutatua haya toka serikali ilipo tangaza elemu bure wazazi wengi wamewaondoa watoto wao mashule binafsi na kuwarudisha shure za serikali na kupelekea kupungua mapato yetu lakini TRA bado kodi zao zipo juu lakini ikumbukwe tunagharamia vitu vingi kama magari,mafuta na maboresho pamoja na vyakula vyote vinaenda katika huduma nasio katika kujinufaisha naiomba serikali ijaribu kuliangalia hili na kutuchukulia wamiliki wa shule binafsi serikali ituchukulie kama watoa huduma kwa kupunguza gharama za kodi", alisema mmiliki wa St Margaret's.

Mbalai na malalamiko hayo mbali mbambali ya wawekezaji Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Murro aliweza kufikia makubaliano ya kikao kazi hicho katika wilaya yake kufanyika tena Septemba 30 mwaka 2019 ili kuangalia ni changamoto ngapi zimefanyiwa kazi na kutatuliwa kabisa kwa wawekezaji katika wilaya yake ya Arumeru.

Awali akifungua kikao kazi hicho mkuu wa wilaya Jerry Murro alieleza kuwa kwasasa wafanyabiashara wanapaswa kujiamini katika hawamu hii ya tano ya uongozi wa docta John Pombe Magufuli kwani tayari ameshaonyesha mwanga wa kuwaweka pampoja wawekezaji na kuanza kujenga bandari kavu,kufufua treni na kujenga barabara za kuonganisha mikoa,miji na majiji na zile za mipakani za kuonganisha mataifa yanayotuzunguka kwa kuweka huduma stahiki kwa wafanya biashara huku akitaka wafanyabiasha wa wilaya yake kutumi fursa zilizopo ili kujikuza kulibiashara na kiuchumi.

Kikao kazi hicho kiliweza kuuzuliwa na watendaji wa idara zote za serikali katika halmashauri hiyo ya Arusha,viongozi wa kisiasa,wawakilishi wa secta za serikali na secta binafsi,wafanya biashara wakubwa nawakati aidha kikao hicho cha wafanya biashara kiliweza kuweka maadhimio mbali mbali ya utendaji ambayo septemba 30 mwaka huu kitatoa mresho wa utendaji na utatuzi wa changamoto walizo zieleza mbele ya viongozi wa serikali.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: