Monday, 3 June 2019

UZINDUZI WA MASHINDANO YA UMITASHUMTA YAMEFANYIKA JIJINI ARUSHA CHINI YA UDHAMINI WA TTCL

 Kutoka katikati ni Afisa Utamaduni Jiji la Arusha Benson Maneno,aliyepo kulia kwake ni Meneja wa TTCL mkoa wa Arusha na Manyara,Brown Japhet
 Meneja wa TTCL mkoa wa Arusha na Manyara,Brown Japhet akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Arusha katika katika uzinduzi rasmi wa michezo ya UMITASHUMTA.
 Meneja wa TTCL mkoa wa Arusha na Manyara,Brown Japhet akimkabidhi mpira Afisa Utamaduni Jiji la Arusha Benson Maneno kama ishara ya uzinduzi rasmi wa mashindano hayo.
 Mwanafunzi kutoka shule ya msingi Ngarenaro Nuru Jofrey Mungure mchezaji wa mpira wa miguu ameihakikishia shule yake kuwa watafanya vizuri hadi kufikia ngazi ya Taifa.
 Mwanafunzi Salha,Mashaka Rajabu kutoka shule ya msingi Ngarenaro amewaomba wazazi wavumbue vipaji vya watoto wao wasivifike kwani michezo ni Afya na Ajira.
Mwanafunzi kutoka shule mojawapo katika Jiji la Arusha anayecheza mpira wa mikono Handball

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Halmashauri ya Jiji la Arusha imeingia ubia na Shirika la simu la  TTCL ,Mkoani Arusha,katika maswala ya mashindano ya michezo  kwa vijana katika shule za Msingi UMITASHUMTA 

Benson Maneno ni Afisa utamaduni katika Jiii la Arusha amesema Michezo hiyo imedhaminiwa na TTCL katika msimu wote wa mashindano ambapo yataanza kesho june 4 na kushirikisha vijana 500 lakini katoka mchujo watachukua vijana 100 peke yake ambao watawaingiza katika timu ya mkoa wa Arusha 

Maneno amesema Halmashauri ya Jiji la Arusha imejipanga kikamilifu kwa mashindano hayo kuhakikisha inafanya vizuri ambapo tamebeba kauli mbiu isemayo "Michezo na TTCL Rudi nyumbani kumenoga"

Kwa upande wake Meneja wa TTCL mkoa wa Arusha na Manyara,Brown Japhet amesema kampuni hiyo imeguswa kusaidia sekta ya michezo katika.Jiji la Arusha kwa kuwa michezo ni sehemu ya ajira na wanamichezo wengi duniani wanamafanikio makubwa kutokana na michezo.

Amesema kupitia michezo hiyo kampuni ya TTCL itajitangaza Kitaifa na kimataifa na amewataka wananchi kutumia fursa hiyo kuitangaza kampuni hiyo ya kitanzania inayoungwa mkono na serikali.

Katika hafla hiyo likiendana na ugawaji wa line za  simu za TTCL  kwa  washiriki ambapo wamepata fursa kujipatia kama sehemu ya wadau muhimu katika kulitangaza kampuni hilo .

No comments:

Post a Comment