Sunday, 2 June 2019

UWT Zanzibar yawataka wana CCM kuwapa ushirikiano Wabunge


Mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti (UWT)Taifa Thuwaiba Kisasi akisalimiana na mwenyeji wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Angelina Malembeka jana,katika mafunzo ya elimu ya ujasiriamali na mikopo pamoja na Daftari la mpiga kura mafunzo yalioandaliwa na Mbunge Malembeka(PICHA NA HERI SHAABAN)
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Angelina Malembeka  akizungumza na Wanawake wa (UWT) katika mafunzo ya kuwapatia elimu ya Ujasiriamali na mikopo pamoja na Daftari la kudumu la Wapiga kura,mafunzo ya yaliandaliwa na mbunge Malembeka jana "katika ukumbi wa Mahonda Wilaya ya Kaskazini B
Mkurugenzi wa Kampuni ya Guru Planet Nickson Martin akitoa mafunzo ya ujasiriamali na elimu ya mikopo kwa Wanawake wa (UWT)wa Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Mafunzo yalioandaliwa na Mbunge Angelina Malembeka wilaya ya kaskazini B

NA HERI SHAABAN,ZANZIBAR

UMOJA wa Wanawake (UWT)  Zanzibar yawataka wana CCM kuwapa ushirikiano Wabunge na wa Wakilishi wa CCM watokanao na Baraza la Wawakirishi, mpaka muda wao utakapofika wa uchaguzi kwa sasa wasiweke mafungu kwa kuwagawa makundi.


Tamko hilo limetolewa  Mahonda Wilaya ya Kaskazini B,Mkoa wa Kaskazini Unguja na mgeni rasmi Makamu  Mwenyekiti wa UWT Taifa  Thuwaiba Kisasi wakati wa mafunzo ya kuhamasisha Daftari la Wapiga kura na utoaji wa Elimu ya mikopo na ujasiriamali,mafunzo yaliyotolewa na Kampuni ya Guru Planet kwa Wanawake wa Kaskazin Unguja,mafunzo hayo  yaliandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Kaskazini Unguja Angelina Malembeka.

"Nawaomba muwaunge mkono Wabunge wenu wa Chama cha Mapinduzi wa majimbo , Viti Maalum na Wawakilishi, wakati wakitekeleza Ilani wakiwa katika majimbo" alisema Kisasi.

Kisasi alisema Chama kinatizama kwa makini Jumuiya zake hivyo wasichafue chama na Jumuiya bali wazipe nguvu Jumuiya hizo katika utekelezaji wa Ilani.

Aidha alisema wale watakaokaidi agizo la Chama na kuanza kampeni mapema majina yao yatakatwa marufuku kuweka makundi wakati yupo mtu katika nafasi hiyo anatekeleza Ilani.

Alielezea  kuhusiana na daftari la kudumu la uboreshaji  Wapiga kura alisema aliwataka Wanawake kujitokeza kwa wingi pindi muda utakapo fika wa kujiandikisha sambamba na kuwamasisha watu walio na sifa kushiriki kujiandikisha.

Akizungumzia elimu ya mikopo alisema mwanamke lazima awezeshwe kiuchumi katika elimu ya ujasiriamali na kukuza soko la biashara.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Angelina Malembeka alisema   
"imefika wakati sasa Wanawake tujikwamue kiuchumi na kukuza soko la  uchumi wa viwanda nchini".

Malembeka aliwataka Wanawake wa mkoa huo kuunga mkono  juhudi za Rais katika utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi na usimamiaji wa miradi ya kisasa.

Aliwataka Wanawake wa mkoa huo kuanzisha viwanda vidogovidogo kuunga mkono juhudi za Rais  John Magufuli pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt.Mohamed Ally Shein katika uchumi wa viwanda.

Naye Mwalimu wa Mafunzo ya ujasiriamali wa Kampuni ya Guru Planet Nickson Martin alisema kampuni ya Guru Planet inafanya kazi mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani.

Martini alisema wao ni washauri elekezi katika masuala ya mikopo  aliwataka Wajasiriamali wabadirike waache kufanya biashara kwa mazoea..

Martin aliwataka wajasiriamali wa mkoa huo kuweka utaratibu wa kufunga hesabu kwa mwezi na kuweka mpango mkakati wa mwezi na mwaka.


Mwisho

No comments:

Post a Comment