Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI Dr.Ntuli Angelile Kapologwe akizungumza na watumishi wa Hospital ya Wilaya ya Chato wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani humo.
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dr. Japhet Simeo akifuatilia kikao wakati Mkurugenzwa Afya alipokuwa akizungumza na watumishi wa Hospital ya Wilaya ya Chato.
 Dr. Fatuma Mrisho akizungumza wakati wa kikao na Mkurugenzi wa Afya alipokuwa akizungumza na watumishi wa Hospital ya Wilaya ya Chato
 Wataalamu toka Ofisi ya Rais TAMISEMI wakifuatilia kikao cha Mkurugenzi wa Afya a na watumishi wa Hospital ya Wilaya ya Chato
Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI Dr.Ntuli Angelile Kapologwe(kwanza kulia) akitoa maelekzo ya jumla wakati wa kuhitimisha ziara yake ya kikazi katika Hospital ya Wilaya ya Chato.
Nteghenjwa Hosseah, Chato

Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI Dr.Ntuli Angelile Kapologwe amesema huduma jumuishi za afya kwa wananchi masikini si jambo hiari bali ni wajibu wa kila mtoa huduma katika vituo vya kutolea huduma za Afya Nchini.

Dr. Ntuli amesema hayo wakati alipokutana na watumishi wa Hospital ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita kuzungumzia masuala mbalimbali ya kiutendaji na namna ya kuboresha utoaji wa huduma za Afya kwa Jamii.

Dr. Ntuli amesema mwananchi masikini hapaswi kubaguliwa kwa sababu tu hawezi kuchangia huduma za Afya ni wajibu wetu kumhudumia kisha kujirdhisha kama kweli hana uwezo wa kulipa kisha kupewa msamaha kwa mujibu wa Sera ya Afya.

“Moja kati ya haki ya msingi za kila binadamu ni kufurahia viwango vya juu vya afya viwezekanavyo na sisi kama watumishi wa Serikali tunalo jukumu la kutoa huduma bora za afya zinazofikika na zinazopatikana kwa watu wote bila ubaguzi.

Msamaha katika huduma za Afya unahusishwa mama mjamzito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano lakini kwa mama yule ambaye ana Bima ya Matibabu inapaswa kutumika ili kuchangia na gharama hizo ambazo zitaenda kusaidia wananchi ambao hawana uwezo hivyo katika hili ni muhimu tuelimishe wananchi ili kuwa na uelewa wa pamoja” Alisema Dr Ntuli.

Aidha Dr.Ntuli aliongeza kuwa msamaha huu pia unalenga wazee wenye zaidi ya miaka sitini na wale wenye magonjwa sugu lakini msamaha huo utatolewa pale ambapo afisa usawi wa jamii wa hospital au kituo husika atajiridhisha pasipo shaka kuwa makundi haya yote yaliyotajwa kwenye msahama hawana kabisa uwezo wa kuchangia huduma za Afya.

“Kila mtoa huduma anapaswa kuelewa vyema kuhusu msamaha na nani analengwa kati msamaha huu, mwananchi yupi anapaswa kuchangia huduma na yupi anapaswa kupewa msamaha na mfahamu fika kuwa utaoji wa msamaha huu si kwa mujibu wa matakwa yetu bali ni Sera ndio imeelekeza hivyo kila mmojawetu atimize wajibu wake katika hili” alisema Dr, Ntuli.

Sambamba na hilo Serikali inaendelea kupanua utoaji wa huduma za afya kila inapowezekana, kuhakikisha upatikanaji wa dawa ni wa uhakika, wataalamu wa afya wanaajiriwa na kuendelezwa kulingana na mahitaji na wanapata motisha: Tunatarajia jitihada hizi zitawezeshe utoaji wa huduma za Afya kuzidi kuimarika kuanzia ngazi ya msingi, ninachowataka ni nyinyi kujituma kwa moyo na kuhakikisha wananchi wanakuwa na Afya njema na mnaokoa maisha ya watanzania alimalizia Dr.Ntuli.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dr. Japhet Simeo amemshkuru Mkurugenzi wa Afya kwa kukutana na watumishi wa Afya, kuskiliza changamoto zao, kutafuta ufumbuzi wa pamoja na kutoa maelekezo ya Serikali katika kuboresha huduma za Afya.

“Nikuhakikishie tu kuwa maelekezo uliyatoa tumeyapokea na tutayafanyia kazi kwa weledi na kufuata miiko ya Taalumu yetu ili kuhakikisha tunafanikisha ile dhana ya upatikanaji wa huduma za Afya kwa wote” alisema Dr. Japhet”
Share To:

Post A Comment: