Sunday, 2 June 2019

TPB BENKI YAMWAGA MIKOPO KWA WAJASIRIAMALI MKOANI TANGA”

 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Banda la Benki ya Posta kwenye maonyesho ya saba ya biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kulia ni MENEJA wa Tawi la Benki ya Posta (TPB) la Tanga Jumanne Wagana
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga Edward Bukombe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Banda la TPB Benki kushoto ni MENEJA wa Tawi la Benki ya Posta (TPB) la Tanga Jumanne Wagana   
MENEJA wa Tawi la Benki ya Posta (TPB) la Tanga Jumanne Wagana aliyevaa koti jeusi akizungumza na wageni mbalimbali waliotembelea banda lao kwenye maonyesho hayo
 MENEJA wa Tawi la Benki ya Posta (TPB) la Tanga Jumanne Wagana kulia akisalimiana na kiongozi wa TCCIA Mkoani Tanga wakati wa maonyesho hayo
 Maafisa wa Benki ya Posta Tawi la Tanga (TPB) kulia wakimsikiliza mmoja wa wakazi wa Jiji la Tanga aliyetembelea Banda lao
MENEJA wa Tawi la Benki ya TPB la Tanga Jumanne Wagana kushoto akimkabidhi zawadi kiongozi wa TCCIA ambao ndio waandaaji wa maonyesho hayo

NA MWANDISHI WETU, TANGA.

WAJASIRIAMALI wadogo na wakubwa wapatao 3400 mkoani Tanga wamenufaika na mikopo kutoka Benki ya Posta (TPB) wenye thamani ya Bilioni 9.1 ambao umewawezesha kujikwamua kiuchumi.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Benki ya Posta (TPB) tawi la  Tanga Jumanne Wagana wakati wa maonyesho ya Biashara ya kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini hapa.

Alisema kwamba mikopo hiyo ilitolewa pia kwenye vikundi mbalimbali, watumishi wa umma na wazee waastaafu kwa mkoa mzima wa Tanga.

Aidha alisema wakati wanaanza kutoa mikopo hiyo mwaka jana waliweza kuitoa kwa wateja 3000 ambao ulikuwa na thamani ya sh.bilioni 8 huku wakiweka lengo la kuwafikia wateja wengi zaidi.

Akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo ni baadhi ya wateja kushindwa kurudisha mikopo hiyo kwa wakati huku wengine wakiwa na mikopo zaidi ya mmoja.

Hata hivyo aliwataka wateja wao kuendelea kutumia huduma zao mara kwa mara kwa sababu mikopo yao wanatoa kwa riba nafuu na huduma nzuri zinazowajali wateja wao.

No comments:

Post a Comment