Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua mizani ya kupima pamba za wakulima katika Kijiji cha Imalanguzi katika Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora tarehe 14 Juni 2019 wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya ufuatiliaji wa chanagmoto ya zao la Pamba. (Picha zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akihutbia
mamia ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Mwabuzo Wilayani Meatu, Mkoa wa Simiyu wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya ufuatiliaji wa chanagmoto ya zao la Pamba, tarehe 14 Juni 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua skimu ya umwagiliaji ya Igurubi iliyopo katika
Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora tarehe 14 Juni 2019 wakati akiwa katika
ziara ya kikazi ya ufuatiliaji wa chanagmoto ya zao la Pamba.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akihutbia
mamia ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Mwabuzo Wilayani Meatu, Mkoa wa Simiyu wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya ufuatiliaji wa chanagmoto ya zao la Pamba, tarehe 14 Juni 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo - Simiyu
Uongozi
wa Wizara ya Kilimo umewasili katika mikoa ya Kanda ya ziwa ili kubaini
changamoto zinazowakabili wakulima wa zao la Pamba na kuzitafutia
ufumbuzi.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameongoza timu hiyo ambapo amezuru
katika mikoa ya Tabora na Simiyu kwenye Wilaya za Igunga na Meatu.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) anatembelea katika Mikoa ya
Shinyanga na Mara huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew
Mtigumwe akizuru katika Mikoa ya Geita na Mwanza.
Akiwa
katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Imalanguzi
Kijiji cha Igurubi Wilayani Igunga, na Kijiji cha Mwabuzo Wilayani
Meatu, Mhe Hasunga amesema kuwa wizara ya Kilimo ipo katika mchakato wa
kutafuta mfumo madhubuti wa ununuzi wa Pamba.
Alisema
mfumo huo punde utakapoelekezwa utatumika lakini ni mfumo ambao utakuwa
maalumu kwa ajili ya kuimarisha na kuboresha sekta ya pamba nchini.
Amesisitiza
kuwa ili kuimarisha kilimo nchini ni wazi kuwa wakulima wanapaswa
kupatiwa Pembejeo za kilimo ambazo ni Mbegu, Mbolea na Viuatilifu.
“Hatuwezi kuwakomboa wakulima kama tutaendelea na uagizaji wa pembejeo
feki ambazo zinawarudisha nyuma wakulima” Alikaririwa Mhe Hasunga
Katika
ziara hiyo yenye lengo la kutambua changamoto ya zao la Pamba, masoko
yake na upatikanaji wa pembejeo, Waziri Hasunga ameeleza kuwa zao la
pamba ni sehemu ya mazao makuu ya biashara nchini hivyo ni lazima
litafutiwe ufumbuzi.
Aidha,
Mhe Hasunga ametumia nafasi hiyo kuwaeleza wananchi katika mikutano
hiyo kuwa Wizara ya Kilimo ipo katika mapitio ya sera ya Kilimo ya mwaka
2013 itakayopelekea kuwa na sheria ya kilimo itakayomnufaisha mkulima
na kulinda rasilimali za kilimo ikiwemo ardhi.
Kadhalika,
amesema kuwa serikali inaendelea na zoezi la usajili wa wakulima huku
akisisitiza umuhimu wa sekta ya umwagiliaji ambayo ikisimamiwa vizuri
itakuwa muarobaini wa kilimo pasina kutegemea msimu wa mvua kwa ajili ya
kilimo.
MWISHO
Post A Comment: