Sunday, 23 June 2019

TCRA WAHITIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA UMMA ARUSHA

 Kaimu Mkuu wa kanda ya Kaskazini Mhandisi Imelda Salum akizunguza na waandishi wa habari kuhusiana na hitimisho la Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa Utumishi wa Umma katika stendi ya kilombero Jijini Arusha,kushoto kwake ni Thadayo Ringo ni mkuu wa kitengo kinachoshughulikia maswala ya watumiaji huduma na bidhaa za mawasiliano (TCRA
 Thadayo Ringo ni mkuu wa kitengo kinachoshughulikia maswala ya watumiaji huduma na bidhaa za mawasiliano (TCRA) akizunguza na waandishi wa habari kuhusiana na hitimisho la Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa Umma katika stendi ya kilombero juzi ijumaa Jijini Arusha.
Kaimu Mkuu wa kanda ya Kaskazini Mhandisi Imelda Salum ,kushoto kwake ni Thadayo Ringo ni mkuu wa kitengo kinachoshughulikia maswala ya watumiaji huduma na bidhaa za mawasiliano (TCRA)baada ya kuhitimisha la Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa Umma katika stendi ya kilombero juzi ijumaa Jijini Arusha.

Thadayo Ringo ni mkuu wa kitengo kinachoshughulikia maswala ya watumiaji huduma na bidhaa za mawasiliano (TCRA)akizungumza na wananchi ambao wapo kwaajili ya kupatiwa huduma kutoka TCRA ,NIDA,UHAMIAJI pamoja na baadhi ya watoa huduma wa makampuni ya simu.

Wananchi waliojitoleza katika stendi ya kilombero wakati wa hitimisho la Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja.

Hali halisi ilivyo katika stendi ya kilombero juzi ijumaa jioni wakati muda ukiwa umeisha bado wananchi wanaonekana ni wengi katika kituo hicho

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Mamlaka ya Mawasiliano nchi TCRA imehitimisha wiki ya Utumishi kwa Umma kwa kutoa huduma za usajili na uhakiki wa laini za simu kwa njia ya vidole.

Imelda Salum ni kaimu mkuu wa kanda ya kaskazini TCRA amesema wananchi ambao wamechukua fomu kwaajili ya kupata vitambulisho vya uraia  ni 4757,laini zilizosajiliwa kwa njia za vidole 2073,laini mpya zilizouzwa ama  kusajiliwa ni 417 hivyo ambapo zoezi hilo limekuwa na manufaa makubwa.

Amesema pamoja na kuhitimisha zoezi bado wananchi waliiendelea kujitokeza kwa wingi ambapo wengi wameiomba Mamlaka hiyo iendelee kubakia eneo la stendi ya kilombero kwaajili ya zoezi hilo

Mhandisi huyo amesema kwa mujibu wa maadhimisho walilazimika kufikia mwisho ambapo amewataka wananchi yeyote yule anayehitaji huduma ya kusajili laini yake aende kwenye ofisi ya mtoa huduma husika ,na kwa wale ambao wanaenda kuanza mchakato wameshauriwa kwenda  kwenye Mamlaka ya vitambulisho vya NIDA

Mhandisi huyo ameainisha Changamoto kubwa ambayo ilijitokeza katika zoezi hilo ni kwa baadhi ya  wananchi wengi hawafahamu namba za vitambulisho vyao,kwani wapo ambao hawafahamu namba zao,wengine walishaajiandikisha  ila hawajapata vitambulisho wanahitaji kupata namba zao ili waweze kusajili laini zao za simu,kuna ambao hawajaanza hata huo mchakato wa kujiandikisha kabisa.

Wapo wananchi wengine kutokana na changamoto mbalimbali hawakuweza kufikiwa na zoezi la uandikishwaji wakati Nida walivyokuwa wanaandikisha katika maeneo ya wananchi amesema hilo ndilo eneo ambalo wameliona linachangamoto.

"Wananchi ni wengi wapo wanahitaji kupata hiduma  lakini kwa vile zoezi letu likikuwa linaishia ijumaa hatukuweza kuwahudumia wananchi wote"

Mhandisi Imelda Salum anesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) haijaweka mkomo wa kusajili laini za simu ilimradi mtumiaji wa hizo laini za simu aweze kuthibitisha anazihitaji zile laini zote kwa matumizi yake binafsi kama unaweza kuthibitisha kwamba unahitaji laini tatu au nne kwa matumizi yako binafsi basi unaweza kusajili.

Juma Marwa ni mwananchi na mkazi wa Sombetini Jijini Arusha ambae alifika katika stendi hiyo kupatiwa huduma amesema  zoezi hilo kwake limekuwa na faida kwani aliweza kupatiwa namba yake ya kitambulisho cha Kitaifa ambapo ameweza kusajili laini zake za simu.

Eva Shayo ni mkazi wa Kwamrombo Jijini Arusha ameiomba Mamlaka ya TCRA pamoja na NIDA kupanga siku nyingine ambayo itawasaidia wao kama wafanyabiashara wa masokoni kupata nafasi nyingine kwaajili ya kuhakiki namba zao kwani wapo wengi ambao hawajaweza kupata namba .

"Ikiwezekana jamani watufuate hadi masokoni maana muda mwingi tunakimbizana na biashara".alisema mama huyo

No comments:

Post a Comment