AFISA Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo kulia akifanya mazoezi na watumishi wa mamlaka hiyo leo(Ijumaa) jioni
 Sehemu ya watumishi wa Tanga Uwasa wakiwa kwenye mazoezi katikati ni Kaimu Afisa Rasilimali Watu wa Tanga Uwasa Theresia Sanga
 Mazoezi yakiendelea
 AFISA Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo kulia akiwa na watumishi wenzake wakishiriki mazoezi hayo
Mazoezi yakiendelea kama inavyoonekana

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) wameanza utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais Samia Suluhu kwa kufanya mazoezi siku tatu kwa wiki baada ya muda wa kazi kwisha.

Mazoezi hayo hufanyika Jumanne, Jumatano na Ijumaa ambayo yameonekana kuwa chachu kwa watumishi ambao wamekuwa wakishiriki

Akizungumza mara baada ya kumalizika mazoezi ya leo Kaimu Afisa Rasilimali Watu wa Tanga Uwasa Theresia Sanga alisema wameamua kufanya mazoezi hayo ili kuweza kuimarisha miili yao na kuiweka imara pia husaidia kupunguza msongo wa mawazo.

Alisema pia kupitia mazoezi hayo mbali ya kuimarisha miili yao lakini pia yanajenga umoja na kuweka kujenga ushirikiano kwenye kazi hali inayosaidia kutekeleza majukumu yao vema.

“Lakini pia mazoezi yanaondoa msongo wa mawazo hivyo ni jambo zuri huku akiwahamasisha watumishi kuhakikisha kila wakati wanashiriki kwani yanafaida kubwa kiafya”Alisema

Awali akizungumza Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Dorrah Killo alisema mazoezi hayo ni mazuri kwa sababu yanawapa umoja na kupelekea kupendana ikiwemo kuongeza hari ya uwajibikaji

Mwisho.
Share To:

Post A Comment: