Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Tanesco mkoa wa Arusha imefanya
Operesheni Maalumu ya kukagua mita zaidi ya 1000 na kubaini baadhi ya watu waliochakachua
mita za umeme ikiwa ni njia ya kukwepa kulipa malipo stahiki ya huduma za umeme
hivyo wamechukuliwa hatua za kisheria.
Afisa Ukaguzi wa Mita Zuberi
Hassan amesema kuwa baada ya kufanya ukaguzi huo wamebaini mita kadhaa ambazo
zimechezewa ili zisiweze kusoma vizuri matumizi ya umeme jambo ambalo ni hujuma
kwa shirika hilo.
Mmiliki wa eneo ambalo lilikaguliwa na
kukutwa na tatizo la mita kuchakachuliwa ,Joseph Shirima amesema
kuwa tatizo hilo lilisababishwa na baadhi ya wapangaji wasio waaminifu kufunga
mita zao hivyo atashirikiana na shirika hilo ili kuhakikisha mita zinazowekwa
zina kuwa na usahihi.
Meneja wa wateja wakubwa Tanesco
Mhandisi Frederick Njavike amesema kuwa shirika hilo limefanya ukaguzi wa
mita zaidi ya 1000 katika maeneo mengi
jijini Arusha ili kujiridhisha na mita zilizopo pamoja na kuchukua hatua
stahiki ikiwemo kusitisha huduma za umeme pamoja na kuchukua hatua Kali za
kisheria ili iwe fundisho kwa wateja wenye tabia ya kuchezea mita
Post A Comment: