NA HERI SHAABAN

TAASISI ya Fahari Tuamke Maendeleo yadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika kwa kusaidia Watoto wanaoishi mazingira magumu pamoja na kuwapa kadi za bima ya Afya.


Madhimisho hayo ya siku ya Mtoto wa Afrika yalifanyika Kata ya Gongolamboto Manispaa ya Ilala mgeni rasmi aliku  wa Ofisa Elimu Msingi Manispaa ya Ilala Elizabeth Thomas aliongoza kugawa vifaa vya shule kwa watoto walio katika mazingira Magumu na kuwapa kadi za Bima ya Afya.


Akizungumza katika  madhimisho hayo   amewataka Wazazi kulinda ndoto za Watoto wao ili waweze kufikia malengo yao ikiwemo kuzingatia elimu.

"Tunaomba wazazi mzingatie ndoto za watoto wenu waweze kufikia malengo yao pia watoto wanatakiwa kusoma wazazi wengi wanachangia kurudisha nyuma ndoto za watoto kutokana na migogoro ya ndoa na familia" alisema Thomas.


Thomas aliwataka wazazi kuitumia vizuri taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo katika kulinda mtoto kama sehemu ya kwanza  ya kumlinda Mtoto .

Aidha aliwataka watoto wazingatie elimu kwani elimu aina mwisho serikali yetu ni sikivu ya awamu ya tano katika utekekezaji wake wa elimu bila malipo.

Akielezea kuhusiana na mimba za utotoni mara nyingi serikali inakosa  ushirikiano kutoka kwa wazazi  kuhusiana na mimba za utotoni amewataka wazazi kutoa ushirikiano kwa serikali.

Amewataka Wazazi Walezi kuzingatia Kauli mbiu ya mwaka huu" Mtoto ni Msingi wa Taifa  endelevu Tumtunze,Tumlinde na   Kumuendeleza"

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo ,Neema Mchau alisema madhimisho hayo yamefanyika katika kata hiyo iliunganisha wadau wa ustawi wa Watoto ,wazazi na walezi wa watoto wa kata Gongolamboto Wilayani Ilala.

Neema alisema siku ya mtoto wa Afrika sio sherehe bali ni kumbukumbu ya maandamano yaliofanywa na watoto  wa Kitongoji cha Soweto Afrika ya Kusini wakiwa na lengo la kudai haki za msingi kupinga vitendo vyote vya unyanyasaji wa watoto walio kuwa  vilivyokuwa vikifanywa na Serikali ya Makaburu Juni 1976.

" Mwaka 1976 watoto hao waliandamana wakiimba nyimbo kwa mabango yenye ujumbe  zinazoashiria madai yao ya msingi maandamano hayo yalipelekea watoto kupoteza maisha" alisema Neema.

Aidha Neema alisema kukithiri kwa sherehe za jadi na vigodoro vinachangia sana mmomonyoko wa maadili kwa watoto  kwa kukesha usiku kucha maeneo ya wazi.

Alisema tabia hiyo imepelekea baadhi ya watoto kukariri maneno mabaya  ya nyimbo na kujifunza tabia zisizofaa kwa jamii.


Pia michezo ya kamari na kubeti,mitaani inasababisha watoto kuiba pesa majumbani na kwenda kucheza wakiamini watapata pesa nyingi .
Share To:

msumbanews

Post A Comment: