Na Timothy Itembe, Mara

Siasa imetajwa kuwa kikwazo moja wapo katika ukamilishaji wa ujenzi wa shule ya msingi Mturu inayojengwa  katika mtaa wa Mkuyuni pamoja na mtaa wa Uwanja wa Ndege.


Akiongea jana kwenye mkutano wa hadhara wa uwanja wa mkuyuni,Chacha Machugu maarufu (Chacha musukuma)  alisema kuwa ujenzi wa shule hiyo ulianza mwezi Mei,2017 kwa nguvu za wananchi lakini  hadi sasa shule hiyo imekwama kukamilika kwasababu ya kisiasa.

Musukuma aliongeza kuwa lengo la kuanziasha ujenzi wa Shule hiyo ni kuepusha watoto kugongwa na magari pindi wanapokuwa wanavuka Barabara itokayo Tarime kwenda Mugumu Serengeti wakielekea shuleni kutafuta masomo.

Musukuma alitaja sababu nyingine kuwa ni pamoja na kuwaondolea kutembea umbali mrefu watoto kwenda shuleni Rebu kutafuta masomo hususani watoto wadogo waliochini ya umri wa miaka kumi  na kurudi chini.

Naye Rhoda Manyinyi alisema kuwa shule hiyo imejengwa kwa nguvu za wananchi na kuwa wamejenga wakati mgumu lakini cha kushangaza serikali haijawaunga mkono ili watoto wakaanza masomo.

Manyinyi alitumia nafasi hiyo kuomba serikali ya wamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kuwaunga mkono wananchi wa mkuyuni pamoja na wa Uwanja wa Ndege ili kuhakikisha kuwa watoto wanapata masomohapo.

Kwa upande wake, Saimon Mwita maarufu Kidevu alisema kuwa wananchi wa Mtaa wa Mkuyuni pamoja na Uwanja wa Ndege wametumia nguvu zao pamoja na mali zao kujenga Shule hiyo  ili kuokoa maisha ya wanafunzi ambao walikuwa wanateseka kwa kugongwa na magari wakati wakienda shuleni Rebu kutafuta masono.

Kidevu alitumia nafasi hiyo kupongeza uongozi wa serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli pamoja na mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Tarime,Elias Ntiruhungwa kukubali wito wa ombi la wananchi kuwaruhusu shule hiyo kujengwa ndani ya mtaa wake ili kupunguza adha kwa wanafuzi wanaotarajiwa kusomea hapo.

Pia Kidevu aliongeza kuwa shule hiyo ikikamilika itasaidia baadhi ya wanafunzi wa kata ya Nkende, kuja kusoma hapo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: