Monday, 10 June 2019

Serikali:Fuvu la Binadamu wa kale kuanza kuonekana julai 17 Mwaka huu

 Katibu mkuu wa wizara ya maliyasili na utalii Profesa Mkenda akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Utalii Karibufear 

Kamishna Mkuu wa Uhifadhi TANAPA Dkt.Allan Kijazi akizungumza wakati wa utoaji wa Tuzo ya Serengeti kuwa Hifadhi bora Barani Afrika na kilele cha maonyesho ya Kimataifa ya Utalii ya Karibufear kwenye viwanja vya TGT Kisongo mkoani Arusha .

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa nchini(TANAPA) Jenerali Msaafu George Waitara  akizungumza wakati wa utoaji wa Tuzo ya Serengeti kuwa Hifadhi bora Barani Afrika na kilele cha maonyesho ya Kimataifa ya Utalii ya Karibufear kwenye viwanja vya TGT Kisongo mkoani Arusha .

Adam Malima mkuu wa mkoa wa Mara akizungumza wakati wa utoaji wa Tuzo ya Serengeti kuwa Hifadhi bora Barani Afrika na kilele cha maonyesho ya Kimataifa ya Utalii ya Karibufear kwenye viwanja vya TGT Kisongo mkoani Arusha

Kutoka kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangala akifuatiwa na Mwenyekiti wa bodi ya Utalii nchini Kamishana General Msaafu George Waitara
Mkurugenzi wa Utalii Shirika la Hifadhi la Taifa Ibrahim Mussa Baadhi ya wahifadhi kutoka Tanapa
Wadau mbalimbali wa Utalii na wafanyakazi wa Bank ya NMB
Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa TANAPA wakifuatilia hotuba na matukio mbalimbali wakati wa kutangaza maadhimisho ya miaka 60 ya Hifadhi ya Serengeti na Bonde la Olduvai julai 17 mwaka huu.
Mkurugenzi wa kampuni ya Matriarch Hill Safari Sophie Augustino 
Mkurugenzi wa kampuni ya Matriarch Hill Safari Sophie Augustino  ambayo inaajiri waongoza Utalii wanawake na kutoa fursa mbalimbali kwa watoto wa kike.

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa tarehe 17 julai nwaka huu kutakuwa na maadhimisho ya miaka 60 ya bonde la Olduvai na Hifadhi ya Serengeti ambapo mamlaka hizo zitaandaa usafiri maalumu kuanzia Karatu kwenda kujifunza na kujionea fuvu la binadamu wa kale.

Ameeleza kuwa Fuvu hilo tangia limegundulika halijawahi kuonekana hadharani na hivyo itakuwa ni fursa kwa Watanzania kuweza kuona na serikali kuongeza wigo wa vivutio vilivyopo.

"Hii ni mara ya kwanza kwa fuvu hilo kuoneshwa na kuwekwa Kwenye makumbusho ya Olduvai na miaka 60 tokea kuanzishwa kwa hifadhi ya Serengeti na kugundulika kwa Fuvu la binadamu wa kale"

Profesa Mkenda amesema Ushindi wa hifadhi ya Serengeti katika tuzo ya kuwa hifadhi bora kabisa katika bara la Afrika kwa mwaka 2019 ambapo ilitangazwa rasmi june mosi nchini Mauritius kwa kura zilizopigwa na wateja na wataalam mbalimbali wa mambo ya utalii duniani na kutambua vivutio vilivyopo na huduma bora zinazotolewa na hifadhi ya Serengeti.

Katika kundi la tuzo hiyo hifadhi bora ya Taifa  barani Afrika kwa mwaka 2019 serengeti ilishindanishwa na hifadhi nyingine tano za bara la Afrika ambazo ni Kalahari ya Botswana,Kitesha Namibia,Kidepo Uganda  Kugi A.Kusini na Masai Mara Kenya.

Amesema Tuzo hiyo ya WTA inayotambulika kwa kuheshimika zadi duniani hutolewa kwa kuzingatia huduma bora zenye viwango vya hali ya juu.

Profesa Mkenda amesema Serengeti imeshinda kutokana na umaarufu wake unaotokana na wingi wa uonekanaji wawanyama wanaohama  kama yumbu na Pundamilia, urahisi wa kuonekana kwa wanyama walao nyama ambao simba,fisimadoa Duma,pamoja na uwanda mpana na nyasi fupi wenye madhari ya kuvutia mito maarufu kama Mara na Gurumeti yenye mamba na viboko wengi.

"Serengeti inakuwa hifadhi ya Pili chini ya TANAPA  kupata tuzo ya WTA ambapo Hifadhi ya Kilimanjaro iliwahi kupata tuzo ya shirika hilo kwenye kipengele cha kivutio bora Barani Afrika kwa miaka 5 mfululizo kuanzia 2015-2018 ambapo awali ilishawahi kupata tuzo hiyo 2013 ushindi huo wa hifadhi ya Serengeti ni heshima kubwa kwa Taifa la Tanzania na pia ni fursa muhimu kuendelea na kutangaza vivutio vyetu vya utalii ili tuweze kupata tuzo nyingi zaidi kwa miaka ijayo na kuvutia watalii wengi nchini mwetu" Alisema Profesa Mkenda.

Akiongea mara baada ya katibu mkuu kutembelea katika mabanda ikiwa ni siku ya kilele cha maonyesho ya kimataifa ya utalii ya karibukilifair 2019 mkurugenzi wa kampuni ya Matriarch Hill Safari Sophie Augustino amesema kuwa kamapuni hiyo itaendelea na mkakati wake wa kuajiri waendesha utalii wanawake kwa lengo la kuonyesha na kuwezesha watoto wa kike kuona utalii siyo sehemu ya wanaume pekee.

Amesema vikwazo alivyovipata yeye hadi kutimiza ndoto zake imempa chachu ya kuona wanawake wengi wakishiriki kama wanaume katika sekta ya utalii na kuwa changamoto zao zinakuwa ni fursa ya kufikia malengo na ndoto zao.

"Nawaomba wadau katika sekta ya utalii na nyingine nchini kuungana nami katika kuhakikisha mtoto wa kike anashiriki kikamilifukatika ujenzi wa taifa na kuepwa msaada wa hali na mali ili waweze kufanikisha ndoto zao"Alisema

Ameongeza kuwa Kampuni hiyo mbali na changamoto imeweza kuajiri wafanyakazi wanawake 4 ambao wamefanya kampuni hiyo kusimama na ndiyo maana wameweza kushiriki katika maonyesho hayo na kuweza kujitangaza na kujitafutia masoko ili kuiboresha kuwa kuwa kubwa na kushindana na makampuni mengine yaliyopo kwa sasa kwenye sekta ya Utalii. 


No comments:

Post a Comment