Friday, 21 June 2019

RC MAHENGE AONGOZA JOPO LA VIONGOZI KUTATUA KERO ZA WANANCHI DODOMA

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr.Binilith Mahenge akizungumza
 MBUNGE wa Jimbo la Dodoma (CCM) na Naibu Waziri Ofisi Ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira akizungumza
 MKUU wa wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi akizungumza
 MKURUGENZI wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi akizungumza
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr.Binilith Mahenge ameongoza jopo la Viongozi wa Wilaya ya Dodoma Mjini kwenye ziara maalum katika ngazi za mitaa kusikiliza kero zinazowakabili wananchi wa Jiji la Dodoma na kuzipatia ufumbuzi kero hizo.

RC Mahenge ameanza ziara hiyo jana katika kata za Ipagala na Nzuguni na kuendelea na ziara leo katika kata za Mpunguzi na Mbabala ambapo amesikiliza kero kubwa za wananchi katika maeneo ya ni Migogoro ya Ardhi,Maji,Umeme,Miundombinu na Masuala ya Afya.

“Kila kiongozi katika eneo lake ahakikishe anakuwa mstari wa mbele katika kusikiliza kero na kutafuta majawabu wa kero hizi za wananchi,si jambo jema kupuuza kero hizi kwasababu sisi tumepewa dhamana na heshima ya kuwahudumia wananchi hawa hivyo basi tumsaidie kwa vitendo Mh Rais Magufuli katika kuhudumia Watanzania”Alisema RC Dr.Mahenge.

Katika ziara hiyo RC Dr.Mahenge ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh.Patrobas Katambi,Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde,Mkurugenzi wa Jiji Ndg Godwin Kunambi na wataalamu kutoka TARURA,TANESCO,TANROADS,SUMATRA na DUWASA.

Aidha Wananchi wa Jiji la Dodoma wamepongeza hatua hiyo ya Viongozi kusikiliza kero za wananchi kwa ukaribu na kuzipatia majibu hali ambayo itapunguza malalamiko mengi waliyonayo wananchi.

No comments:

Post a Comment