Sunday, 23 June 2019

RC Kagera "sitakubali vitendo vya ukatili wa kijinsia na wakati wataalamu wapo"
Na Clavery Christian Bukoba.

Mkuu wa mkoa kagera brigedia jeneral Marco Elisha Gaguti amesema kuwa baada ya kupokea kesi nyingi ya ukatili wa kijinsia ofisini kwake yeye kama mkuu wa mkoa ameamua kuanzisha kampeni ya kusikiliza kero na matatizo ya wanakagera ambayo itawashirikisha wataalamu kutoka taasisi mbalimbali za kiserikali ambapo kwa pamoja wataweza kuzishughulikia.

Rc Gaguti amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ili kutoa taarifa kwa wananchi kujitokeza wakati kampeni hiyo itakapo anza ambayo inatarajiwa kuanza tarehe 27 june 2019 mpaka tarehe 29 june 2019 ambapo amesema kuwa kwa mda wa siku tatu wamejipamga kuhudumia zaidi ya watu elfu mbili ndani ya siku hizo tatu na kusema kuwa kampeni hiyo itajumuisha wataalamu takribani 45 na wanasheria 20 pamoja na takukuru, dawati la jinsia na maafisa ustawi wa jamii ambapo wataweza kumsikiliza kila mtu kwa makini na kumpatia msaada wa kisheria kulingana na changamoto yake.

Aidha amesema kuwa kampeni hii itaendeshwa kwa kutumia mfumo wa kiditali ili kuwezesha kuweka kumbukumbu vizuri na kuwa watafanya kazi bila kuchoka ampabo amesema kuwa ofisi ya mkuu wa mkoa na ofisi ya mkuu wa wilaya pia zitakuwepo na kuhakikisha haki inatendeka huku akisema kwamba kampeni hii inatarajiwa kuwalenga sana wanawake has a walionyanyaswa na kudhurumiwa aridhi zao baada ya kuwapoteza wapendawa wao.

No comments:

Post a Comment